Mbunge
wa Viti Maalum Chadema, Rose Kamili, ambaye pia ni mke wa Katibu Mkuu
wa chama hicho Dk. Wilbrod Slaa, akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada
ya kukamatwa kwa madai ya kukutwa akigawa rushwa kwa wapigakura leo
jioni katika Kijiji cha Kitawaya, Kata ya Luhota, wakati ikiwa ni siku
ya mwisho kabla ya kufanyika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga kesho. Hadi
tunakwenda mitamboni Rose alikuwa bado anashikiliwa Kituo Kikuu cha
Polisi mkoa wa Iringa.
Rose akipandishwa kwenye karandinga la Polisi
Post a Comment