Walevi nchini Kenya wamekuwa wakilalamika kuhusu
matumizi ya kifaa malum cha kupima kiwango cha pombe walichokunywa
madereva wa usiku wanapokuwa wakiendesha magari wakiwa walevi.
Sheria ya kulewa na kuendesha magari nyakati za
usiku imekuwa kali kwani polisi wanasisitiza kuwa lazima madereva wa
usiku wapimwe ikiwa wamekunywa pombe kupita kiasi hali inayotishia
usalama wao barabarani.
Tangu kifaa cha ''Alco-Blow'' au
kifaa kinachotumiwa kupima kiwango cha pombe alichokunywa dereva kuanza
kutumika kama njia ya kudhibiti ulevi barabarani mezi kadhaa iliyopita,
utata umeibuka kuhusu usalama wa kukitumia kiafya kwani kinatumiwa na
madereva wengi.
Lakini polisi wamesema kuwa watu wasiwe na
wasiwasi kwani tahadhari zote zimechukuliwa ili kuzuia tisho lolote la
afya kwa watumiaji.
Na pia sio lazima uweke mdomo wako kwenye kifaa bali unapuliza tu na kinachukua vipimo.
Usalama barabarani
Usalama barabarani umekuwa tatizo kuu nchini
Kenya ambapo takriban watu elfu tatu hufa kutokana na ajali za
barabarani kila mwaka .
Idara ya trafiki imesema kuwa asilimia 85 ya
ajali hizo husabishwa na makosa ya kibinadamu yanayochangiwa kakubwa na
ulevi kupindukia.
Hayo yote ni kwa mujibu wa sheria kali ya kunasa
madereva walevi. Ni dhahiri kuwa kuendesha gari ukiwa mlevi ni hatari
kubwa , lakini kuna wale ambao hawajafurahishwa na jinsi seriklai
imetimiza sheria ya kunasa madereva walevi.
Kumekuwa na mjadala mkali nchini Kenya ikiwa
kifaa cha AlcoBlow ni salama au la kutokana na watu zaidi ya mmoja
kukitumia wakati polisi wanapofanya ukaguzi wao katika vizuizi vya
barabarani
Ujanja wa walevi
Josephat Baraza ni meneja wa baa moja jijini
Nairobi, anasema kuwa wakati operesheni ya kurejesha usalama barabarani
ni muhimu, imeleta hasa kwa wauza mpombe na wanaomiliki mikahawa.
Lakini wamekuwa wajanja nao kwani wamezindua
huduma ya kuajiri madereva wanaoendesha magari ya wateja wa baa yao na
kuwarejesha nyumbani kwa njia salama baada ya kunywa pombe na kuendesha
magari yo huku wakijozolea balaa.
Walevi wamejaribu juu chini kujinasua kutoka
katika mtego wa polisi wanaoshika doria barabarani. mitandao wa jamii
kama Facebook na Twitter kuonya wenzao kutopitia bara bara waliko
polisi.
Licha ya hayo, Charles Keitany ambaye ni afisa
mkuu anayesimamia usalama wa barabara kuu za Kenya anasema lazima
wataendela na operesheni ya kuwanasa madereva walevi.
Si mara ya kwanza polisi wa Kenya kutumia kifaa
vya kupima kiwango cha ulevi, kila mara hatua hii imepata pingamizi kali
kutoka kwa umma ambao wamepeleka kesi mahakamani kutaka kifaa hicho
kutohalalishwa.
Mahakama moja jijini Nairobi ilitupilia mbali kesi hiyo.
Kawa sasa kuna Wakenya ambao wananunua kifaa
hicho kwa matumizi yao binafsi lakini mkuu wa polisi anyesimima barabra
kuu za Kenya anashauri unaponunua kifaa cha kibinafsi lazima upate cheti
cha kudhibitisha uhalali wake kutoka kwa shirika la kitaifa
linalodhibiti ubora wa bidhaa.
BBC
Post a Comment