Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KIJANA AUAWA KWA MAWE NA KISHA KUCHOMWA MOTO BAADA YA KUIBA PIKIPIKI WILAYANI KAHAMA..!!

Kijana mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25-30 ameuawa kwa kupigwa mawe kisha kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kukamatwa na pikipiki ya wizi Katika kijiji cha kagongwa Wilayani Kahama mkoani Shinyanga. 
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa nane Mchana mara baada ya marehemu kuiba Pikipiki hiyo yenye no T634 CNK Aina ya SanLG mali ya Patrick Seba mkazi wa Nyahanga Mjini Kahama ambayo imeibiwa jana Asubuhi Maeneo ya shule ya Kahama Musilim ikiwa imeegeshwa na dereva wake aitwaye Shija Zacharia.
Kwa mujibu wa Mmiliki wa pikipiki hiyo Bwana Seba Ameiambia redio Kahama fm Kuwa alipewa taarifa na dereva wake ambpo aliamua kutoa tarifa ya upoteza pikipiki hiyo kwa waendesha bodaboda wa mjini Kahama na Kagongwa.
Amesema wakati anatoka Kagongwa kutoa taarifa ndipo akakutana na vijana wawili ambao walikuwa wanaiendesha pikipiki hiyo kuelekea Kagongwa ambapo aliamua kuwafuatilia na kwamba aliwapata katika kijiji hicho.
Baada ya kuwasogelea aliizima pikipiki hiyo kwa kutumia remote kwani wakati inaibiwa ilikuwa imezimwa kwa kutumia Remote ambapo walianguka china na Kuanza kukimbia huku wananchi wakaanza kumshambulia mmoja kwa mawe hadi kumuua huku mwingine akifanikiwa kukimbia kusikojulikana.
Hata hivyo jeshio la Polisi wilayani Kahama limedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mwili wa marehemu ulipelekwa kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifdadhia maiti kwenye hospitali ya Wilaya ya kahama.
Kwa takribani miezi Miwili na Nusu sasa watu wa wanne wameuawa kwa kuchomwa na moto katika kijiji hicho kwa madai kuwa wamechoshwa na kukithiri kwa wimbi la wizi katika Kijiji hicho na maeneo jirani. 
 
chanzo: Dunia Kiganjani
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top