Na Francis Godwin Blog
WANANCHI
wa Ludewa mkoani Njombe wamempongeza Rais Dr Jakaya Kikwete
kwa hatua yake ya kuwashirikisha wananchi wa maeneo husika katika
suala la utatuzi wa mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi
Hatua
ya wananchi hao kumpongeza Rais Dr Kikwete imekuja huku
ikiwa ni siku tatu zimepita toka mbunge wao wa jimbo la Ludewa
Deo Filikunjombe ,mbunge wa jimbo la Kyela Dk. Harrison
Mwakyembe na mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi John Komba kurejea
nchini kutoka Malawi katika kikao cha usuluhishi wa mgogoro wa
mpaka kati ya Malawi na Tanzania
Wakizungumza na
mwandishi wa habari hizi wananchi hao akiwemo Yohana Haule
walisema kuwa hatua ya Rais Kikwete kutumia wananchi wenye
kushughulikia suala hilo ni hatua ya kupongezwa kwani wabunge hao
ni wawakilishi wa wananchi hivyo kila kinachoendelea
kitawafikia mapema wananchi wa maeneo ya mpakani Malawi na Tanzania.
Haule alisema
kuwa imani na matumani ya wana Ludewa ni kuona mbunge
wao amewawakilisha katika suala hilo na kuwa hawana shaka
na uwakilishi wake na wanaamini watapewa mrejesho wa
kila kinachoendelea katika suala hilo.
Hivyo
alisema kwa sasa hofu ambayo awali wananchi wa kando ya ziwa
Nyasa walikuwa nayo juu ya mgogoro huo wa mpaka kati ya Tanzania na
Malawi imeanza kutoweka kutokana na mbunge wao Filikunjombe
kuzunguka maeneo yote ya Mwambao na kufanya mikutano na kuwaondoa
hofu juu ya hilo.
Huku Sarah
Haule mbali ya kumpongeza Rais Kikwete kwa hatua hiyo pia
alimpongeza mbunge Filikunjombe kwa jitihada mbali mbali za kuwaletea
maendeleo wananchi wa Ludewa huku akimtaka mbunge huyo kuendelea
na msimamo wake katika kuwawakilishi wana Ludewa bungeni .
Post a Comment