KAMATI
ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
(TASWA) ilifanya kikao chake cha kwanza chini ya uenyekiti wa Juma Pinto
juzi Jumatatu Machi 10, 2010 jijini Dar es Salaam na kujadiliana kuhusu
masuala mbalimbali.
1; MAFUNZO
Kikao
kilikubaliana kuelekeza nguvu katika mafunzo kwa wanachama wake na kwa
kuanzia kamati iliagiza sekreterieti ya TASWA ihakikishe inasimamia hilo
kwa nguvu zote ili kuboresha uwezo wa namna ya kuripoti michezo
mbalimbali hasa kwa waandishi chipukizi.
Katika
hilo bajeti maalum itaandaliwa kwa ajili ya kuona namna ya kushirikiana
na wadau mbalimbali watakaosaidia mafunzo hayo ikiwemo Chama cha
Kimataifa cha Waandishi wa Habari za Michezo (AIPS).
2;Media Day
Kama
inavyojulikana kwamba kila mwaka TASWA inaandaa bonanza maalum
likihusisha waandishi na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari
hapa nchini.
Mwaka
huu Kamati ya Utendaji imepanga lifanyike Mei 10 jijini Dar es Salaam
katika eneo ambalo lina fukwe nzuri. Hivyo tayari watu maalum
wameshateuliwa kufanya utaratibu wa mahali litakapofanyika.
Pia
mazungumzo na wadhamini mbalimbali kuhusu bonanza hilo litakaloenda
sambamba na sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
yameanza na yana muelekeo mzuri, ambapo litashirikisha waandishi wa
habari na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari 2,000.
3;Tuzo za Wanamichezo Bora
TASWA
imeunda kamati maalum ya kusimamia tuzo hiyo na kuifanya iwe bora
pengine kuliko za miaka iliyopita. Majina ya kamati hiyo tutayatangaza
baada ya wote kuwa wameshapatiwa barua zao za uteuzi na kuzijibu. Tarehe
ya tuzo ni baada ya kamati kukutana na ndiyo itakayopendekeza kulingana
na majukumu iliyopewa.
4; Marekebisho ya Katiba
Pia
kikao kilikubaliana kuelekeza nguvu katika marekebisho ya katiba ya
chama. Katika kufanikisha hilo imeundwa kamati maalum kwa ajili ya jambo
hilo. Majina ya kamati hiyo pia yatatangazwa baada ya wote kuwa
wameshapewa barua zao na kujibu kwa maandishi.
5;SACCO’S
Kwa
kuwa suala hili lilishapitishwa kwenye Mkutano Mkuu wa chama Desemba
2012, kikao kilikubaliana lifanyiwe kazi na utekelezaji uanze sasa.
Utaratibu
unaandaliwa kuhusiana na jambo hilo baada ya kupata mwongozo kutoka
vyama vya ushirika, kisha wanachama wa TASWA watajulishwa na wale
watakaopenda kujiunga watapewa maelekezo kwani hilo ni jambo la hiyari
kwa yule atakayependa.
6: Uhai wa chama
Suala
la uhai wa chama lilichukua nafasi kubwa, hivyo utaratibu maalum
utawekwa kuhamasisha waandishi wa habari za michezo hasa wale wa mikoani
kujiunga na chama.
Ili
kuweka mkazo jambo hilo, baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya
TASWA na baadhi ya wanachama watapewa fursa kwa ufadhili wa chama
kusafiri maeneo mbalimbali mikoani kuhamasisha waandishi wa huko
kujiunga na chama.
Ahsante.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
12/03/2014
Post a Comment