Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KIKAO CHA MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA WAKUU WA MAGEREZA AFRIKA KITAKACHOFANYIKA MSUMBIJI JULAI 2014 CHAFANYIKA NCHINI AFRIKA KUSINI

    
photoMwenyekiti wa Umoja wa Magereza Afrika, Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Afrika Kusini, Nontsikelelo Jolingana akitoa hoja ya kufungua rasmi Kikao cha Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Magereza Afrika unaotarajiwa kufanyika Nchini Msumbiji Julai 2014. Kikao hicho kimefanyika hivi karibuni Mwishoni mwa mwezi Februari, 2014 Nchini Afrika Kusini na kuhudhuliwa na Nchi Wanachama ikiwemo Tanzania.
image
Washiriki wa Kikao cha Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Magereza Afrika wakiendelea na majadiliano ya Kikao hicho Jijini Johanesberg, Afrika Kusini hivi karibuni. Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Magereza Afrika unaotarajiwa kufanyika Nchini Msumbiji Julai 2014
. image_1
Baadhi ya Washiriki wa Kikao toka Nchi Wanachama Barani Afrika wakifuatilia kwa makini mjadala katika Kikao cha Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Magereza Afrika unaotarajiwa kufanyika Nchini Msumbiji Julai 2014.
image_2.
Baadhi ya Wakuu wa Magereza Afrika wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga rasmi Kikao cha Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Magereza wa Afrika unaotarajiwa kufanyika Nchini Msumbiji Julai 2014. Kikao hicho kimefanyika mwishoni mwa mwezi Februari 2014 Jijini Johanesberg Afrika Kusini(wa kwanza kushoto mstari wa mbele) ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Afrika Kusini, Nontsikelelo Jolingana(wa kwanza kushoto mstari wa nyuma) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Hamunyela( wa pili kulia mstari wa mbele) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Msumbiji, Dkt. Eduardo Mussanhane (wa kwanza kulia mstari wa nyuma) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja. image_3Sekretarieti Kuu ya Umoja wa Vyombo vya Urekebishaji/Magereza Afrika wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Urekebishaji/Magereza Afrika mara baada ya kufungwa rasmi kwa Kikao cha Maandalizi ya Kikao cha Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Magereza unaotarajiwa kufanyika Nchini Msumbiji Julai 2014(wa tatu toka kulia mstari wa nyuma) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza)
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top