Mkurugenzi
Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Vicent
Assey akizungumza na wataalam walioshiriki katika mkutano uliojadili namna ya
kuhusisha masuala ya lishe katika mpango wa kunusuru kaya masikini na
zinazoishi katika mazingira hatarishi unaoratibiwa na TASAF

Baadhi ya
washiriki wa mkutano uliondaliwa na TASAF kujadili namna bora ya kuhusisha
masuala ya lishe katika mpango wa kunusuru kaya masikini sana nchini
wakimsikiliza mkurugenzi Mtendaji wa TASAF , Ladislaus Mwamanga ( hayupo
pichani) wakati alipofungua mkutano huo kwenye ukumbi wa CEEM ,jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi
Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Vicent
Assey akizungumza na wataalam walioshiriki katika mkutano uliojadili namna ya
kuhusisha masuala ya lishe katika mpango wa kunusuru kaya masikini na
zinazoishi katika mazingira hatarishi unaoratibiwa na TASAF
=========== =========== ============
TASAF NA MKAKATI WA KUKABILIANA NA TATIZO
LA LISHE DUNI NCHINI.
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF
kupitia Mpango wa kunusuru kaya masikini sana na zilizo katika mazingira
hatarishi ,PSSN umekutana na wadau wa sekta mbalimbali za kiserikali kujadili
namna ya kushirikiana katika kuhakikisha kuwa suala la lishe bora linapewa
umuhimu mkubwa ili kupambana na tatizo la utapiamlo hususani kwa watoto nchini.
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa
wadau wa sekta za afya na lishe kwenye ukumbi wa CEEMI jijini DSM,Mkurugenzi
Mtendaji wa TASAF ,Ladislaus Mwamanga amesema jitihada zaidi zinapaswa
kuelekezwa katika kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuboresha afya kwa
kutumia lishe bora hususani kwa watoto ili kujenga makuzi sahihi ya ubongo wao.
Mwamanga amesema TASAF kwa upande wake
imeweka mfumo imara wa kuwahusisha watalaamu wake ambao wamesambazwa katika
maeneo mbalimbali nchini kote na kutoa rai ya kuwahusisha katika kampeni
mbalimbali za kuwaelimisha wananchi juu ya matumizi sahihi ya vyakula kwenye maeneo
husika.
Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF
amesisitza kuwa pamoja na TASAF kuanza utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya
masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi ambapo suala la lishe ni moja
ya vipengele muhimu, ni vema sekta nyingine pia zikashirikiana na taasisi yake
katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata elimu sahihi juu ya namna bora ya
kuboresha lishe hususani kwa watoto na akinamama wajawazito.
Mwamanga
pia ametoa rai kwa wataalam kutumia mbinu mbalimbali za kuwasilisha ujumbe
sahihi wa masuala ya lishe na kuzisambaza kwa walengwa jambo litakalosaidia
kupambana na tatizo la kudumaa kwa makuzi na ubongo kwa watoto ambapo kwa sasa
inakadiriwa kuwa asilimia 42 ya watoto nchini wamedumaa kimakuzi.
Mapema
akizungumza katika mkutano huo ulioshirikisha wadau kutoka Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii,Wizara ya mifugo na Uvuvi ,Wizara ya Kilimo,Taasisi ya Lishe na
Chakula na wataalamu kutoka TASAF,Mkurugenzi wa uratibu wa Shughuli za Serikali
katika Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Obeyi Assery amesema suala la kudumaa
katika makuzi ya mtoto ni tatizo kubwa nchini ambalo linapaswa kutatuliwa kwa
nguvu za wadau mbalimbali .
Naye mkurugenzi msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Vicent Assey amepongeza jitihada za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF kwa kubuni mpango wa kunusuru kaya masikini na zinazoishi kwenye mazingira hatarishi ambapo suala la lishe litawekewa msukumu mkubwa kama moja ya vigezo vya kuzisaidia kaya zitakazoingizwa kwenye mpango huo mkubwa wa aina yake.
Post a Comment