Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi
……………………………………………………………….
Jopo
wa wang’amuzi vipaji limetangaza majina ya wachezaji 36 waliopataikana
katika mchakato wa maboresho ya Taifa Stars ulioshirikisha mechi za
mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Kaimu
Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Salum Madadi amesema jopo hilo liling’amua vipaji 143 katika mchakato,
lakini waliochukuliwa kwa sasa ni hao 36 tu.
Amewataja
wachezaji waliochaguliwa katika mchakato huo kwa upande wa makipa ni
Abdulaziz Khatib Haji (Mjini Magharibi), Abubakar Abbas Ibrahim (Tanga),
Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara) na Mtindi Kheri Ali (Kaskazini Unguja).
Kwa
upande wa mabeki wa pembeni waliochaguliwa katika mchakato huo ambao upo
chini ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager ni Edward Peter Mayunga
(Kaskazini Pemba), Hussein Moshi (Tabora), Omari Kindamba (Temeke) na
Shiraz Abdallah (Ilala).
Post a Comment