“PRESS RELEASE” TAREHE 17.03.2014.
- MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.
- MWENDESHA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.
GARI
LENYE NAMBA ZA USAJILI T.182 AVL AINA YA TOYOTA NOAH LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA DEREVA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MBAKI AMOS (42) MKAZI
WA KIJIJI CHA USHIRIKA LILIACHA NJIA NA KUPINDUKA NA KISHA KUSABABISHA
KIFO CHA DEREVA HUYO MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA
MAKANDANA –TUKUYU.
AJALI
HIYO ILITOKEA TAREHE 16.03.2014 MAJIRA YA SAA 16:16 JIONI HUKO KATIKA
KIJIJI NA KATA YA MASOKO, TARAFA YA PAKATI, WILAYA YA RUNGWE MKOA WA
MBEYA KATIKA BARABARA YA TUKUYU/LUANGWA.
AIDHA
KATIKA AJALI HIYO MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MESHACK ISACK
(19) MKAZI WA MASOKO ALIJERUHIWA NA AMELAZWA HOSPITALINI HAPO. CHANZO
CHA AJALI NI MWENDO KASI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO
KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
MWENDESHA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MBOZI.
MWENDESHA
PIKIPIKI MMOJA AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA LAKE WALA MAKAZI YAKE
ALIYEKUWA AKIENDESHA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.266 CSJ AINA YA
KING LION ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI YENYE
NAMBA ZA USAJILI T.496 BGG AINA YA TOYOTA NOAH ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA
DEREVA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA TIMOTH WILSON.
AJALI
HIYO ILITOKEA TAREHE 16.03.2014 MAJIRA YA SAA 19:30 USIKU KATIKA KIJIJI
CHA HANSEKETWA, KATA NA TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA
MBEYA, BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA.
CHANZO
CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA
SERIKALI WILAYA YA MBOZI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA TARATIBU ZA KISHERIA
ZINAFANYIKA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO
KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment