Mwenyekiti
Mtendaji wa Tume ya kudhibiti ukimwi nchini (TACAIDS) Dkt. Fatuma
Mrisho akifungua semina ya mahakimu na maofisa wa polisi kutoka mikoa ya
Dae es Salaam, Pwani na Morogoro pamoja wanasheria wa serikali
iliyoandaliwa na tasisi hiyo kwa watendaji wa Serikali hivi karibuni
katika ukumbi wa mikutano (Serengeti) jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya washiriki wa semina wakimsikiliza Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya
kudhibiti ukimwi nchini (TACAIDS) Dkt. Fatuma Mrisho wakati akifungua
semina ya mahakimu, maofisa wa polisi kutoka mikoa ya Dae es Salaam,
Pwani na Morogoro pamoja wanasheria wa serikali iliyoandaliwa na tasisi
hiyo kwa watendaji wa Serikali hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano
(Serengeti) jijini Dar es salaam.
(Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO)
……………………………………………………..
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Maambukizi
ya virusi vya ukimwi (VVU) yanazidi kupungua mwaka hadi mwaka Tanzania
kitu ambacho kinaipa faraja ya tasisi ya Serikali inayosimamia masuala
ya HIV/AIDS nchini.
Kauli
hiyo ilitolewa na Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya kudhibiti ukimwi
nchini Dkt. Fatuma Mrisho alipokuwa akifungua semina iliyoandaliwa na
tasisi hiyo kwa watendaji wa Serikali hivi karibuni katika ukumbi wa
mikutano (Serengeti) jijini Dar es salaam.
Washiriki
wa semina hiyo walikuwa ni mahakimu, maofisa wa polisi kutoka mikoa ya
Dae es Salaam, Pwani na Morogoro pamoja wanasheria wa serikali.
Semina
hiyo ililenga kuwajengea uwezo watendaji wakuu wanaosimamia na
kutekeleza sheria ya ukimwi ya 2008 katika kutimiza majukumu yao ya kila
siku kwa kufuata sheri, kanuni na taratibu kwa wanaohitaji msaada wa
kisheria.
Dkt.
Mrisho alisema takwimu zinaonesha kuwa kwa ujumla maambukuzi ya ukimwi
yamepungua kwa kiasi kikubwa nchini ambapo zinaonesha kuwa Tanzania Bara
na Visiwani kuanzia mwaka 2003 hadi 2004 yalikuwa ni asilimia 7.
Mwaka
2007 hadi 2008 maambukizi yalishuka mpaka kufikia asilimia 5.7 na mwaka
2011 hadi 2012 kiwango hicho kilipungua zaidi na kufikia asilimia 5.1
ambacho ni kiwango cha kitaifa, wakati Tanzani Bara pekee kiwango cha
maambukizi ya VVU ni asilimia 5.3 zaidi ya kiwango cha kitaifa.
Taswira
hii ya kupungua kwa maambukizi ya VVU ni tumaini jema kwa nchi
inayolenga kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 kwani nguvu kazi
inaonekana kuendelea kuimarika na inawezekana kujenga uchumi imara kwa
maendeleo endelevu.
“Kila
mtu kwa namna moja au nyingine anaguswa na ugonjwa wa ukimwi maana
hakuna ukoo, kijiji, wilaya na mkoa usio na mtu anayeishi na VVU na
hivyo hadi nchi nzima inaguswa na hali hiyo” alisema Dkt. Mrisho.
Kwa
kuzingatia hali hiyo, Dkt. Mrisho amewaasa washiriki hao wa semina na
wananchi kwa ujumla kuwa VVU kwa asilimia 80 huambukizwa kwa njia ya
ngono, hivyo waache ngono zembe zembe na kusimamia maadili ya kazi yao
na ya kijamii ili maambukizi ya ukimwi yaweze kupungua na kufikia
kiwango cha asilimia sifuri hadi kufikia mwaka 2015 ambayo ni nia na
lengo la TACAIDS na Serikali kwa ujumla.
Naye
Mkuu wa Kitengo cha Sheria TACAIDS Elizabeth Kaganda alisema kuwa watu
wanaoishi na VVU ni binadamu kama binadamu wengine ni lazima
waheshimiwe wapate mahitaji yao ya kila siku na tiba, mwathirika naye
anapaswa kumlinda mtu mwingine asipate ugonjwa wa ukimwi.
Kwa
upande wake Jaji Mstaafu kutoka nchini Kenya Violet Mavisi alisema kuwa
ni wajibu wa mtu mmoja mmoja kama raia, vyombo vya dola na serikali kwa
ujumla kujali haki za binadamu, kuzisimamia na kuzitekeleza kulingana
na sheria za nchi ikiwemo haki ya kuishi, kumiliki ardhi, kuoa, kolewa
na kuwa na familia na haki nyinginezo zinazotambulika kikatiba ndani ya
nchi husika.
Jaji
huyo Mstaafu Kavisi alisisitiza kuwa haki zote anazotakiwa kuzipata mtu
mwingine kwenye jamii usika, ni haki hizo hizo anatakiwa kupata mtu
anayeishi na virusi vya ukimwi.
Mpaka
sasa Tanzania kwa hali ya maambukizi ya ukimwi mikoa inayoongoza kwa
watu wanaoishi na kuishi na VVU nchini ni 10 ikiongozwa na Njombe,
Iringa, Mbeya, Shinyanga, Ruvuma, Dar es Salaam, Rukwa, Pwani, Katavi na
Tabora.
Post a Comment