Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MABEHEWA YA 'TRENI YA MWAKYEMBE' YAANGUKA...!!!

Mvua zilizonyesha usiku wa kuamkia jana zimesababisha injini  ya treni kutoka Stesheni kwenda Ubungo Maziwa, kuacha njia na kusababisha mabehewa kuanguka.
Mabehewa hayo yalianguka katika eneo la Gerezani, kutokana na utelezi katika njia ya treni.
Msemaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL),  Midladjy Maez alisema tukio la kuanguka kwa mabehewa hayo,  lilitokea saa 11 alfajiri ya jana wakati treni hiyo ikienda kuchukua mabehewa.
Alisema usafiri wa treni wa jana jioni, ungeendelea kuwepo kama kawaida, kwani jitihada za kuyanyanyua mabehewa hayo, zingekamilika na wananchi walitakiwa wasiwe na wasiwasi.

Maeneo mengi ya jiji, yaliathiriwa na mvua za jana, hususani barabara ambazo miundombinu yake  ni mibovu.
Barabara inayotoka makaburi ya Shekilango kwenda  Ubungo, imeathiriwa na mvua na kusababisha magari na pikipiki kushindwa kupita, kutokana na shimo kubwa lililopo katika barabara hiyo. 

Waendesha pikipiki katika eneo hilo, walilalamikia Wakala wa Barabara (TANROADS) kushindwa kutengeneza barabara hiyo, licha ya wao kutoa malalamiko muda mrefu. 

 “Mvua imetuharibia, tunalazimika kuweka miguu juu ya pikipiki na abiria anaweka miguu kwenye mapaja yetu ili tupite, tunateseka sana na hili shimo,” alisema mmoja wa madereva hao.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top