Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RITA KUSHIRIKIANA NA SHULE KUTOA VYETI VYA KUZALIWA WANAFUNZI

Hivi karibuni Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ulizindua zoezi la Usajili na Kutoa vyeti katika Shule za Msingi katika Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam. Zoezi hili  ni sehemu ya utekelezazji wa Mkakati wa Usajili wa Watoto walio na Umri kati ya Miaka 6-18 ( 6-18 Birth Registration Initiative) uliobuniwa ili kukabiliana na changamoto ya wananchi wengi kutosajiliwa na kuwa na vyeti vya kuzaliwa.
Katika zoezi hili, RITA inashirikiana na Manispaa ya Ilala kupitia Idara ya Elimu. Kila shule imeteua mwalimu mmoja anayeratibu Usajili katika shule husika na Wanafunzi wasio na vyeti wamapewa fomu za maombi zitakazojazwa na wazazi wao na baada ya hapo hurejeshwa RITA kwa ajili ya uhakiki na kuandaa vyeti. Baada ya vyeti kukamilika, vitapelekwa kwa Mwalimu Mratibu ambaye atavigawa kwa wanafunzi husika.
Katika wiki mbili za kwanza za utekelezaji, mwamko umekuwa mkubwa sana kwani Jumla ya wazazi 16,500 wameshachukua fomu kwa ajili ya kuomba kupata vyeti vya kuzaliwa vya watoto wao na mpaka sasa zaidi ya fomu 1649 zimeshajazwa na kurejeshwa RITA ambazo ni kutoka shule 35 . Jumla ya shule za Msingi 105 zinashiriki katika zoezi hili zenye jumla ya wanafunzi 139,808.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka shule mbalimbali, wazazi na walezi wengi wameonyesha kufurahia zoezi hili kwani huduma zimesogezwa katika maeneo yao pamoja na utaratibu mzima unaotumiwa katika kuhakikisha kila mtoto anapata cheti cha kuzaliwa. Vyeti vinavyotolewa kwa watoto  ni vya kawaida kama vinavyotolewa katika ofisi zozote za RITA na taratibu zote za uhakiki hufanyika kabla ya mwanafunzi kupewa cheti. 
Kwa mujibu wa Takwimu, ni wananchi asilimia 23 tu wamesajiliwa na kupata vyeti nchini ikiwa ni idadi ndogo sana kulinganisha na umuhimu wa Vyeti vya kuzaliwa kwa kila mwananchi. Tunaamini kwamba mkakati huu utakuwa sehemu ya suluhisho ya changamoto hii na unatamewa kuenezwa katika Wilaya nyingine za Mkoa wa Dar es Salaam kuanzia Mwezi Juni mwaka huu. Vile vile utaratibu  unaandaliwa ili kuweza kuzihushisha shule za Sekondari
Tunawahamasisha wazazi wajitokeze kuwasajili watoto katika shule za msingi wanazosoma ili kuwapata vyeti vya kuzaliwa. Hakuna sababu ya mwanafunzi yoyote kutokuwa na cheti cha kuzaliwa katika eneo zoezi hili linatekelezwa kwani huduma imesogezwa karibu na maeneo wanayoishi. Ikumbukwe kwamba watoto wanaopata vyeti sasa watakuja kuvitumia kujiunga na elimu ya sekondari, kupata nafasi ya kusoma katika Vyuo Vikuu, kupata mikopo ya Masomo elimu ya juu, kupata kazi, kupata kitambulisho cha Taifa wakifikisha miaka 18, kufungua akaunti, kupata pasi ya kusafiria na matumizi mengine.
Phillip Saliboko
Afisa Mtendaji Mkuu – RITA
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top