Stori: Mwandishi Wetu, DODOMA
Wasichana wanaofanya biashara ya kujiuza katika maeneo mbalimbali mjini hapa wameelezea neema iliyowafikia kufuatia kujikusanyia pesa ndefu kutoka kwa baadhi ya wabunge wa Bunge la Katiba ambao wanadaiwa kuwalipa vizuri.
Wasichana wanaofanya biashara ya kujiuza katika maeneo mbalimbali mjini hapa wameelezea neema iliyowafikia kufuatia kujikusanyia pesa ndefu kutoka kwa baadhi ya wabunge wa Bunge la Katiba ambao wanadaiwa kuwalipa vizuri.
Wakizungumza na Ijumaa kwa nyakati tofauti, wadada hao ambao baadhi
wanatokea Mikoa ya Dar, Arusha, Mbeya na kwingineko walisema kipindi
hiki wanakiita ni cha mavuno kwao kwani waheshimiwa hao si watu wa
kulipa pesa ndogo wanapowaopoa.
“Yaani sasa hivi ni kipindi cha mavuno, wateja ni wengi na wanalipa
vizuri tofauti na kipindi cha nyuma. Kwa mfano ukibahatika kumpata
mjumbe wa bunge hili linaloendelea sasa, mbona utafurahi na roho yako!
Wanalipa vizuri ile mbaya.
“Kipindi cha nyuma unaweza kulala na mtu akakulipa shilingi 30,000 au
20,000 lakini sasa hivi ni 50,000 kwenda juu, hakuna longolongo,
tusipojenga safari hii basi tena,” alisema msichana mmoja
aliyejitambulisha kwa jina la Husna ambaye kiwanja chake kikuu cha
biashara ni eneo Chako ni Chako.
Mwingine ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini akidai yuko
Dodoma bila ndugu zake walioko Dar kujua alisema: “Unajua hii biashara
inakuwaga na usumbufu sana, unaweza kuchukuliwa na mtu asikulipe lakini
sasa hivi wateja wetu wakuu ni hawa wabunge, wengine wametugeuza nyumba
ndogo zao kabisa.”
Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa, biashara hiyo
sasa imeshika kasi kiasi kwamba baadhi ya waheshimiwa humalizia posho
zao za siku kwa kuzitumbua na madadapoa hao.
Mwandishi wetu alifanya doria siku za wikiendi maeneo ya Chako ni
Chako, Mwenga Bar na zaidi katika kumbi za starehe kama vile Club 84 na
Maisha na kushuhudia magari yakipaki na kupakiza wasichana kisha
kuondoka.
Gazeti hili linatumia nafasi hii kuwaasa waheshimiwa kufanya
walichokifuata bungeni na kuacha michepuko isiyokuwa na maana na wale
wasichana walioona njia sahihi ya kutafuta maisha bora ni kwa kujiuza,
wajue kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha yao.
CHANZO:IJUMAA
Post a Comment