Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa Lefoord Simba, mtoto wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, wakati alipofika nyumbani kwa Waziri Masaki jijini Dar es Salaam, leo kutoa pole. Picha na OMRMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, wakati alipofika nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam, leo kutoa pole kwa kufiwa na mtoto wake, Lefoord Simba. Mazishi yatafanyika kesho kwenye Makaburi ya Kinondoni. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia
Simba, wakati alipofika nyumbani kwa Waziri Masaki jijini Dar es Salaam,
leo kutoa pole kwa kufiwa na mtoto wake, Lefoord Simba. Mazishi
yatafanyika kesho kwenye Makaburi ya Kinondoni. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akijumuika na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini Mkapa, Waziri
mstaafu (wa pili kulia) Mjumbe wa Nec Wilaya ya Busega, Chegeni (kulia)
na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, wakizungumza jambo
wakati wakijumuika kwa pamoja katika maombolezo ya msiba wa Lefoord
Simba, mtoto wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba,
Masaki jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR
Post a Comment