Hii
imetokea Marekani ambapo mama huyu mwenye umri wa miaka 32 akiwa ni
mjamzito, aliamua kuliendesha gari hili na kuliingiza kwenye bahari kwa
makusudi huku watoto wake wakipiga kelele kwamba mama anajaribu
kutuua.Watoto wa Mwanamke huyu ambae imeripotiwa kwamba bado yuko
hospitali akifanyiwa vipimo vya matatizo ya akili, ambao wana umri wa
miaka mitatu, tisa na 10 walichukuliwa na Idara ya watoto na familia
kwenye jimbo la Florida baada ya kupata matibabu.Watoto hawa wote
walikuwemo kwenye gari hili lililolengeshwa baharini na mama yao ambae
anadai alikua anakwenda kwenye sehemu salama ambayo mume wake
walieachana asingeweza kuwafata au kujua waliko.
Wakati
hili tukio linatokea alikuepo karibu Mtalii raia wa Canada ndio maana
video ya tukio na hizi picha zimepatikana zikionyesha kila kitu.
Huyu ni
miongoni mwa watu waliojitokeza kuokoa baada ya kusikia kelele za mtoto
aliekua ndani ya gari akisema ‘mama yetu anatuua’


Post a Comment