Mtaalamu
wa Hali ya Hewa Bw. Hassan Khatib Ame akitoa ufafanuzi wa kitu kwa
wanafunzi wa Skuli ya Kombeni walipotembelea Ofisi ya Mamlaka ya Hali ya
Hewa iliopo ndani ya Uwanja wa ndege wa Zanzibar ikiwa ni pamoja na
kuadhimisha siku ya Hali ya Hewa Duniani iliyo adhimishwa leo.
Afisa
Usalama wa Anga Bw. Rashid Omar Mselem akiwafahamisha kitu wanafunzi wa
Chuo cha Uwalimu Chukwani kuhusiana na usalama wa Anga na Hali ya Hewa
pindi inapokuwa mbaya, katika kuadhimisha siku ya Hali ya Hewa Duniani.
………………………………..
Na Miza Kona – Maelezo Zanzibar
Wanafunzi
wa vyuo na sekondari wameitaka jamii kuwa na mwamko wa kufuatilia
taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya hali ya Hewa pamoja na kutembelea
vituo hivyo ili kuweza kujua na kupata taarifa za mwenendo wa hali ya
hewa Nchini.
Kauli
hiyo wameitoa leo huko katika ofisi za Mamlaka hiyo ziliopo Uwanja wa
Ndege Zanzibar katika Maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani,
wamesema jamii imekuwa haina mwamko mzuri katika kufuatilia taarifa za
hali ya hewa nchini.
Wamesema
kuwa kila siku jamii inatakiwa kujua na kufuatilia taarifa hizo ili
kuweza kufahamu hali ya hewa ilivyo ili kuepukana na majanga na matatizo
yanaweza kutokea ambapo mamlaka hiyo hutoa taarifa.
Aidha
wanafunzi hao wamewataka wanafuzi wenzao kutembelea katika vituo vya
Mamlaka hiyo kwenda kusoma kwa vitendo na kuona shughuli hizo
zinavyotolewa.
Wanafunzi
hao wametembelea sehemu mbali mbali na kuona jinsi shuguli za kituo
hicho zinavyofanyika ikiwepo sehemu ya usalama wa Anga, kipima joto,
kipima mvua, kipima upepo, pamoja utabiri wa hali ya hewa.
Wakitoa
maelezo kwa wanafunzi maafisa mbali mbali wa Mamlaka hiyo wamesema kuwa
huduma nyingi zinazoendeshwa nchini huwa zinashirikiana na Mamlaka ya
Hali ya Hewa kwa taarifa za hali ya hewa ili kuendesha kazi zake.
Wamefahamisha
Mamlaka ya Hali ya Hewa hushirkiana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
jinsi ya kuingia kutoka kwa ndege nchini na namna ya kuwasiliana katika
uendeshaji shughuli wa zake.
Aidha
wamefahamisha kuwa Mamlaka hutoa taarifa zake kwa kutumia vipimo mbali
mbali viliopo nchini vikiwemo kipima ju, kipima upepo pamoja na kipima
mvua na kutoa taarifa jamii jinsi ya hali ya hewa ilivo na itakavyokuwa
nchini.
Nae
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Mohammed Khamis Ngwali , amesema
vijana wanatakiwa kubadilika na kuchukua tahadhari za kukabiliana na
mabadiliko ya hali ya hewa ili kizazi kijacho kiweze kufaidi dunia yenye
mazingira bora.
Hata
hivyo Shirika la Hali ya Hewa linawahamasisha vijana katika kujihisha
na masuala ya hali ya hewa ili kupata maarifa na uelewa na hatua za
kuchukua katika kipindi cha hiki cha mabadiliko ya hali ya hewa duniani.
Amesema
hatua hii muhimu ikichukuliwa na vijana italeta ustawi wa kizazi cha
sasa na kijacho kwa kujenga jamii iliyo imara baadae pamoja na kuokoa
dunia kwenye majanga yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa nchini.
Maadhimisho
ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani hufanyika kila ifikapo tarehe 23 Machi,
kauli mbiu ya mwaka huu ni ushirikishwaji wa vijana katika Masuala ya
Hali ya Hewa.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
Post a Comment