Na Magreth Kinabo –Maelezo
Umoja
wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba la Tanzania Kwanza wasema
kwamba Mhe. hotuba ya Rais,Jakaya Kikwete aliyoitoa wakati wa
uzinduzi wa Bunge Maalum la Katiba ,haikururuga wala
kuingilia mchakato wa kupata Katiba Mpya ,bali alitoa maoni na ushauri
kama kiongozi wa nchi.
Aidha
wajumbe hao wamesema Rais hakuingilia kanuni za bunge hilo
zilizopitishwa, hakubadilisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na hakupiga
kura kwenye vifungu vya Katiba.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa wajumbe hao, Said Nkumba katika
mkutano na waandishi habari uliofanyika kwenye ukumbi wa waandishi wa
habari wa Bunge mjini Dodoma.
Nkumba
ambaye aliambatana na baadhi ya wajumbe wengine watano , ambapo
alisema hotuba hiyo imeweka wazi faida na hasara za mifumo yote ya
Muungano wa Tanzania kwa hoja ili Watanzania wawe nnnnnna fursa pana ya
kutafakari na kuamua
“ Rais ametimiza kauli yake ya kushawishi kwa hoja na si kulazimisha,” alisema Nkumba.
Aliongeza
kuwa alichokifanya Rais katika hotuba yake ni kama kiongozi mkuu wan
chi mwenye hekima na busara na uchungu wa nchi yake na kutambua dhamana
aliyopewa na Watanzania wote bila kujali makundi ameelezea faida na
hasara za mifumo ya Serikali iliyowasilishwa kwenye hotuba ya
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba.
“
Rais katupa moyo na kutuhimiza tumalize kazi haraka na tuifanye kwa
weledi huku tukiweka maslahi ya taifa mbele. Hata pale alipotoa maoni na
ushauri kuhusu baadhi ya vifungu bado alisisitiza kwamba umamuzi wa
mwisho ni wetu sisi wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba,” alisisitiza.
Nkumba
alifafanua kuwa dhana ya kuichambua na kuikosoa Rasimu ya Mabadiliko
ya Katiba si kumdhalilisha Mwenyekiti wa Tume na Wajumbe wake. Hivyo
msingi mzima wa kutolewa rasimu hiyo ni kwamba wananchi waichambue,
kuikosoa ,kuboresha na kuirekebisha na hata ikibidi kuibadilisha na
mwisho kuipigia kura.
Alisema
rasimu hiyo haikuletwa kama Msahafu wala Bibilia Na ndiyo maana
zimewekwa hatua mbili baada ya kazi ya tume kumalizika ,ambazo ni bunge
hilo na kura ya maoni ya wananchi.
Aliwataka wajumbe wa bunge hilo kushirikiana ili kuweza kuifanya kazi hiyo.
Wajumbe
wa bunge hilo wa Tanzania Kwanza wapo takribani 400 na watatoka katika
makundi mbalimbali ,ambaomsimamo wao ni kushawishi kwa hoja na wala
hawatalazimisha.
Post a Comment