Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka Wilaya ya Moshi Mjini(MNEC) Kamanda wa vijana UVCCM Bw Agrey Marealle Akila kiapo cha utii kwa CCM wakati wa kusimkwa kuwa Kamanda wa vijana wa CCM wilayani humo mbele ya mgeni rasimi Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mboni Mhita(hayuko pichani)
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka Wilaya ya Moshi Mjini(MNEC) Bw Agrey Marealle akiwa amekalishwa kwenye kigoda huku akiwa na ngao na mkuki mara baada ya kusimikwa kuwa Kamanda wa vijana UVCCM wilayani humo na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mboni Mhita(hayuko pichani)
Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mboni Mhita(kushoto) akimvalisha kofia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka wilaya ya Moshi Mjini Bw Aggrey Marealle kuwa Kamanda wa Vijana wa CCM wilayani humo Mjini katika halya iliyofanyika viwanja vya CCM katab ya Njoro.
Mkamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mboni Mhita(kushoto) akimkabidhi mkuki Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka wilaya ya Moshi Mjini Bw Aggrey Marealle katika hafla ya kumsimika kuwa Kamanda wa Vijana wa UVCCM wilayani humo katika sherehe ya kumsimika iliyofayika katika viwanja vya CCM kata ya njoromjini humo.
======= ======= =======
Marealle apewa tena Ukamanda wa Vijana wa CCM Moshi Mjini
*Ahimiza mshikamano kwa wanaCCM
MJUMBE wa halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi, (CCM), kupitia Moshi Mjini, mkoani Kilimanjaro, Aggrey Marealle, amesema mshikamano miongoni mwa wanachama wa chama hicho ndiyo pekee utakaopelekea chama hicho kufanya vyema katika chaguzi zijazo.
Bw. Marealle aliyasema hayo juzi mjini Moshi, wakati wa hafla ya
kusimikwa kwake kama kamanda wa vijana wa umoja wa vijana wa CCM,
(UVCCM), wa wilaya ya Moshi Mjini kwa kipindi cha pili cha miaka
mitano, hafla iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa tawi la wakereketwa
la Marealle lililopo Kata ya Bondeni, Moshi Mjini.
"Changamoto kubwa ambayo CCM imekuwa ikikumbana nayo nyakati za
kuelekea chaguzi mbali mbali ni kutokuwa na mshikamano jambo ambalo
mara nyingi hutokana na makundi ndani ya chama, ni vyema tukaepuka
hili na msamiati wetu mpya uwe ni mshikamano, hapa tutashinda",
alisema.
Aidha alitoa wito kwa wananchi hususan wanachama wa CCM kutokutumia
changamoto za kimaisha walizonazo kama sehemu ya maamuzi katika
kuchagua viongozi na mstakabali mwingine wa kisiasa.
Katika hafla ya uzinduzi wa tawi hilo la wakereketwa, Bw. Marealle
alisema kada ya vijana ni nguzo ya Taifa ambayo haina budi kulindwa
kwa kuhakikisha maswala yanayowahusu yanapewa kipaumbele ili wasikate
tamaa.
Akihutubia katika hafla hiyo ambayo ilienda sanjari na kusimikwa
makamanda wapya wa UVCCM Kata zote za Moshi Mjini, Makamu Mwenyekiti
wa UVCCM Taifa, Mboni Mhita, alisema kuwa kazi kubwa ya makamanda wa
vijana wa CCM ni kuwaunganisha vijana, kubaini kero zao na
kuzishughulikia kwa wakati.
Bi Mhita alielezea kazi zingine kuwa ni pamoja na kuwasaidia vijana
kupata ajira za zikiwemo zile za kujiajiri wenyewe pamoja na kutoa
ushauri kwa vijana unaohusiana na mwelekeo wa kisiasa na kimaisha kwa
ujumla.
"Kwa kufanya hivi mtakuwa mnaweka nguzo imara ya Taifa kwa ajili ya
miaka mingi ijayo", alisema na kutoa wito kwa vijana kuwa tayari
kupokea ushauri watakaopata kutoka kwa makamanda hao wapya wa vijana.
Aidha aliwaasa vijana kuiepusha na matumizi ya dawa za kulevya pamoja
na anasa zilizopitiliza ambapo alisema mambo hayo yanachangia kwa
kiasi kikubwa kupunguza ari na nguvu kazi ya Taifa.
Post a Comment