Makamu
Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula akionyesha mfano wa
karatasi la kupiga kura kwa wanachama wa CCM wanaoishi kwenye kitongoji
cha Ulete,Kijiji cha Muwimbi mkoani Iringa .
Mgombea
wa kiti cha Ubunge jimbo la Kalenga kwa tiketi ya CCM Ndugu Godfrey
Mgimwa akiomba kura kwa wakazi wa kitongoji cha Ulete ,kijiji cha
Muwimbi mkoani Iringa ambapo aliwaambia tusikilize sera za kuleta
maendeleo na si porojo zisizo na tija kwa Taifa letu.
Katibu
wa UWT CCM Arusha mjini Ndugu Rehema Mohamed akiwahutubia wakazi wa
kitongoji cha Ulete kijiji cha Muwimbi na kuwaambia Mgimwa atasukuma
maendeleo ya Jimbo hilo na atakuwa muwakilishi mzuri wa jimbo hilo kwa
wananchi Bungeni na kwa madiwani.
Mwakamu
Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula akihutubia viongozi na
Mabalozi 26 wa CCM waKata ya Ifunda,kijiji cha Mfukulembe ambapo
aliwasihi kuwa makini na zoezi zima la upigaji kura na kutupilia mbali
kauli za vyama pinzani zinazosema zitalinda kura kwa helkopta kwani kila
chama kinatoa wakala wake wa kusimamia wakati wa zoezi la kupiga
kura.Makamu Mwenyekiti CCM (Bara) aliendelea kuhutubia bila kujali mvua.
Baadhi
ya Viongozi wa CCM kata ya Ifunda wakiangaia mfano wa karatasi la
kupigia kura ambapo wameshauria kusimamia watu wao kushiriki kupiga kura
siku ya tarehe 16 March 2014.
Godfrey
Mgimwa mgombea wa kiti cha ubunge jimbo la Kalenga kupitia CCM
akihutubia viongozi na mabalozi 26 wa CCM wa kata ya Ifunda kijiji cha
Mfukulembe na kuwaambia kwa kutumia ilani ya uchaguzi ya CCM ambapo
atavipa kipaumbele elimu, afya , na ujenzi wa barabara.
Post a Comment