Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akifungua mkutano wa 58 wa
Kamisheni kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW) Mkutano huu wa wiki mbili
unafanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, na unawakutanisha
wanawake wa kada mbalimbali kutoka Serikali Kuu na Asasa za Kiraia.
Akifungua mkutano, Katibu Mkuu, pamoja na mambo mengine amewataka
wanawake kuendelea kutetea fursa za kijinsia, kupinga ubaguzi wa aina
zote na kuhakikisha kwamba sauti ya wanawake na watoto wa kike
inaendele kusikika katika ajenda mpya za maendeleo baada ya 2015. Kulia
kwake ni Muwakilishi wa Kudumu wa Ufilipino katika Umoja wa Mataifa,
Balozi Libran Cabactulan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mkutano .
Ujumbe
wa Tanzania katika Mkutano huu, unawahusisha washiriki kutoka pande
zote za Muungano, Tanzania Bara na Visiwani. Pichani ni Bi. Asha Ali
Abdulla, Katibu Mkuu, Wizara ya Uwezeshaji, Maendeleo ya Jamii, Vijana,
Wanawake na Watoto, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Tuvako
Manongi, Muwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika
Umoja wa Mataifa, Mhe. Jaji Imani Daud Aboud kutoka Mahakama ya Rufaa
ya Tanzania, na Bi. Joyce Mlowe, kutoka Wizara ya Katiba na Sheria
wakifuatilia hotuba ya ufunguzi.
Sehemu
ya Ujumbe wa Tanzania kutoka kulia Bi. Halima Abdulrahman Omar,
Mtaalamu wa Masuala ya Jinsia, Wizara ya Uwezeshaji, Maendeleo ya Jamii,
Vijana, Wanawake na Watoto- Zanzibar, Bi Mhaza Gharib Juma, Mkurugenzi
wa Mipango, Sera na Utafiti, Wizara ya Uwezeshaji, Maendeleo ya Jamii,
Vijana, Wanawake na Watoto- Zanzibar, na Bi. Ellen Maduhu, Afisa wa
Uwakilishi wa Kudumu anayeshughulikia Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la
Umoja wa Mataifa inayohusika na Masuala ya Maendeleo ya Jamii na Haki za
Binadamu.
Na Mwandishi Maalum
Ikiwa
imebakia miezi michache kufikia kilele cha utekelezaji wa Malengo ya
Maendeleo ya Millennia ( MDGs), Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban
Ki Moon amewataka wanawake kuendelea kupigania haki zao pamoja na za
mtoto wa kike.
Mkuu
huyo wa Umoja wa Mataifa, ametoa wito huo siku ya jumatatu, mbele ya
mamia ya wanawake kutoka mataifa mbalimbali duniani kote ambao wapo
hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kuhudhuria mkutano wa 58 wa
Kamisheni kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW).
Tanzania
inawakilishwa katika mkutano huu ambao ni wa wiki mbili na wajumbe
kutoka pande zote za Muungano – Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.
“
Mnajukumu kubwa mbele yenu” akasema Katibu Mkuu. Na kuongeza,
imebakia miezi michache kufikia hitimisho la MDGs, na katika kipindi
hiki lazima pia tubainishe ajenda za maendeleo baada ya 2015.
Ninategemea sana busara zenu na kujituma kwenu katika kuwasilisha
kwenye meza, sauti za wanawake na watoto wa kike”.
Ban Ki
Moon, amewaeleza wanawake hao kutoka makundi mbalimbali ya jamii
kuanzia Serikalini hadi Asasai za kiraia kuwa, alikuwa pia anawategemea
katika kupigania na kutetea haki za binadamu kwa wote .
“
Hatutawezi kufika mahali pakuwa na dunia yenye hadhi kwa wote mpaka
pale tutakapotokomeza tofauti zote za kijinsia. Nipo pamoja nanyi”
akabainisha Katibu Mkuu huku akisisitiza kwamba usawa wa kijinsia
na uwezeshwaji wa wanawake ni moja ya vipaumbele vyake.
Ajenda
kuu itakayojadiliwa katika mkutano huu wa 58 wa CSW ni mafanikio na
changamoto za utekelezaji wa MDGs. Pamoja na ajenda washiriki wa
mkutano huu pia watakuwa na mikutano ya pembezoni yenye maudhui tofauti
lakini yote ikilenga katika utekelezaji wa MDGs.
Katika
hotuba yake ya ufunguzi, Katibu Mkuu alianisha baadhi ya mafanikio ya
utekelezaji wa MDGs, kama vile ongezeko la watoto wanaokwenda shule
hasa wa kike, kupungua kwa vifo vya watoto wachanga muda mfupi baada ya
kuzaliwa na kupugua kwa pengo la ajira kati ya wanawake na wanaume.
Hata
hivyo akasema, katika eneo la ajira, bado wanawake ni wahanga wa malipo
duni, mazingira magumu ya kazi, huku wakikosa fursa ya pensheni, bima
ya afya na sheria za kazi zinazowalinda.
“
Tumetoka mbali, lakini bado tunasafari ndefu tunahitaji vitendo zaidi
na sera zinazowajengea uwezo Zaidi wanawake, tunahitaji kuwaona
wanawake wengi zaidi serikalini. Nafasi za wanawake katika mabunge
zimeongezeka katika mataifa mbalimbali ingawa bado kuna tofauti kubwa
za uwakilishi katika ngazi zote” akasisitiza.
Eneo
ambalo amelitaja kuwa bado halijatekelezwa vizuri ni eneo la
usafi. Akasema kila mwaka watoto 800.000 chini ya miaka mitano hupoteza
maisha kwa ugonjwa wa kuharisha. Zaidi ya watu 2.5 bilioni wanakosa
huduma sahihi za usafi.
Kama
hiyo haitoshi zaidi ya watu bilioni moja wanajisaidia matika maeneo ya
wazi. “ tukiongeza utoaji wa huduma za usafi , na kuacha kujisaidia
maeneo ya wazi. Hapana shaka tutapunguza sana magonjwa na uchafuzi wa
mazingira na kuboresha zaidi usalama wa wanawake na watoto wa kike
ambao mara nyingi wamo katika hatari kubakwa kwa sababu tu ya ukosefu
wa vyoo safi na salama”.
Post a Comment