Mkuu
wa mkoa wa Njombe Kapeteni Mstaafu Aseri Msangi akiweka jiwe la msingi
ujenzi wa tanki la maji lililopo Mwongolo Makete Mjini.
Ujenzi wa tanki la maji Mwongolo Makete mjini ambao umewekwa jiwe la msingi na mkuu wa mkoa wa Njombe.
Mkuu
wa mkoa wa Njombe Kapteni mstaafu Aseri Msangi (katikati) akielekea
kwenye ujenzi wa mradi wa maji Mwongolo Makete mjini kwa ajili ya kuweka
jiwe la msingi, kulia ni mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro
na kushoto ni katibu tawala msaidizi upande wa maji mkoa wa Njombe Bw.
Christopha Nyandiga.
Meneja
Mamlaka ya maji Makete mjini Bw. Yonas Ndomba akisoma taarifa ya ujenzi
wa tanki la maji Mwongolo, Makete mjini mbele ya mkuu wa Mkoa.
Mkuu
wa mkoa wa Njombe kapt. Mstaafu Aseri Msangi akimsikiliza meneja wa maji
Makete mjini akisoma taarifa, kushoto kwake ni mkuu wa wilaya ya Makete
Mh. Josephine Matiro.
Meneja
wa mamlaka ya maji makete mjini, Bw. Yonas Ndomba akimkabidhi taarifa
ya ujenzi wa tanki la maji la Mwongolo Makete mjini Mkuu wa mkoa wa
Njombe Kapteni mstaafu Aseri Msangi.
Tanki la Maji lililopo Mwongolo ambalo linatumika sasa kama linavyoonekana.Picha zote na Edwin Moshi, Makete.
Post a Comment