Mtihani kwa ajili ya watu
wanaotaka kuwa mawakala wa wachezaji wanaotambuliwa na Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Aprili 3 mwaka huu saa 4
kamili asubuhi ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (FIFA).
Kwa wanaotaka uwakala huo
wanatakiwa kujisajili ambapo watapewa kanuni mbalimbali za FIFA na TFF
ili waweze kujiandaa kikamilifu kwa mtihani huo utakaokuwa na sehemu
mbili. Sehemu ya kwanza ya mtihani huo ni maswali kutoka FIFA wakati
nyingine ni kutoka TFF.
Tanzania ina mawakala watatu tu wa
wachezaji wanaotambuliwa na FIFA. Mawakala hao ni Ally Saleh, John
Ndumbaro na Mehdi Remtulla.
Post a Comment