Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof.
Ibrahim Lipumba akiiunga Mkono Azimio la Kutunga na Kupitisha kanuni za
Bunge Maalum la katiba leo Mjini Dodoma. |
Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba na Naibu Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Jenista Mhagama akiunga Mkono Azimia la Kutunga na Kupitisha kanuni za Bunge Maalum la katiba leo Mjini Dodoma. |
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Panya Ally Abdalah(Mwenye mtandio wa Zambarau) akiiunga Mkono Azimia la Kutunga na Kupitisha kanuni za Bunge Maalum la katiba leo Mjini Dodoma. |
Mwenyekiti wa Muda wa Bynge Maalum la Katiba akiwaleza jambo wajumbe wa Bunge Hilo kabla ya kuahirishwa mpaka kesho jioni na Kuwataka wale wanaotaka kuchukua fomu ya uenyekiti kuanza kuzichukua leo. |
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Frederick Msigala akiunga Mkono Azimio la Kutunga na Kupitisha kanuni za Bunge Maalum la katiba. |
(Picha na Hassan Silayo-MAELEZO)
……………………………………
Na Jovina Bujulu, Maelezo Dodoma.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wameunga mkono azimio la kutunga na kupitisha kanuni za bunge Maalum la katiba.
Wakiongea
kwa nyakati tofauti ndani ya ukumbi wa bunge baadhi ya wajumbe
waliopata nafasi waliwataka wajumbe wengine kuunga mkono na kupitisha
azimio hilo kwa maslahi ya taifa na wananchi kwa ujumla.
Aidha
wajumbe hao waliwapongeza wajumbe walio katika kamati ya kuandaa rasimu
ya kanuni itakayotumika kuongoza bunge hilo kwa kazi waliyoifanya tangu
kuanza kwa semina ya marekebisho ya kanuni hizo.
Pia
wajumbe walimpongeza mwenyekiti wa muda wa bunge hilo Bw. Pandu Ameir
Kificho kwa kuongoza bunge hilo la uandaaji wa kanuni kwa umakini na
busara.
Naye
mwenyekiti wa muda wa bunge hilo Bw. Pandu Ameir Kificho aliwataka
wajumbe wenye nia ya kugombea uenyekiti wa Bunge hilo kwenda kuchukua
fomu za maombi za nafasi hiyo katika ofisi za katibu wa bunge.
Kuhusu
suala la Makamu mwenyekiti wa Bunge hilo Bw. Kificho alisema kwamba
nafasi hiyo itajazwa pale mwenyekiti atakapopatikana kwani matakwa ya
sheria ya bunge hilo yanataka nafasi hizo kuwa na wawakilishi toka pande
zote mbili za Tanzania.
“Tunasubiri
kumpata mwenyekiti kwanza kabla ya makamu mwenyekiti kwani sheria
inasema iwapo mwenyekiti atatoka Tanzania bara basi makamu wake atatoka
Zanzibar na vilevile kama mwenyekiti atatoka Zanzibar basi makamu wake
atatoka Tanzania bara.” Alisema Kificho.
Mpaka
jioni ya leo wajumbe 4(nne) wameshachukua fomu hizo wakiwamo Samwel
Sitta, Theresia Huviza, John Lifa Chipaka na Hashim Rungwe.
Post a Comment