Na Boniface Wambura, TFF
Waamuzi na waamuzi wasaidizi 22
wameteuliwa kushiriki semina na mtihani wa utimamu wa mwili kwa robo ya
kwanza ya mwaka huu itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Machi 14
hadi 16.
Semina hiyo inashirikisha waamuzi
wote wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na
wale wa ngazi ya juu (elite) kutoka Tanzania Bara za Zanzibar.
Waamuzi hao ni Charles Simon
(Dodoma), Dalila Jafari (Zanzibar), Ferdinand Chacha (Mwanza), Hamis
Chang’walu (Dar es Salaam), Helen Mduma (Dar es Salaam), Israel Mujuni
(Dar es Salaam), Issa Vuai (Zanzibar), Janeth Balama (Iringa), Jesse
Erasmo (Morogoro), John Kanyenye (Mbeya) na Jonesia Rukyaa (Bukoba).
Josephat Bulali (Zanzibar), Lulu
Mushi (Dar es Salaam), Martin Saanya (Morogoro), Mfaume Nassoro
(Zanzibar), Mohamed Mkono (Tanga), Mwanahija Makame (Zanzibar), Ngaza
Kinduli (Zanzibar), Oden Mbaga (Dar es Salaam), Ramadhan Ibada
(Zanzibar), Samwel Mpenzu (Arusha) na Waziri Sheha (Zanzibar).
Wakufunzi wa semina hiyo ambao wanatambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ni Joan Minja na Riziki Majala.
Post a Comment