Naibu
Waziri wa Fedha mhe Mwigulu Nchemba amehutubia kikao cha pamoja cha
bunge la ACP na EU katika mji wa Strasbourg nchini Ufaransa.
Katika
hotuba yake, mhe Mwigulu alianza kwa kukishukuru chombo hicho kwa ajili
ya msimamo wake usioyumba kwenye maswala ya amani akitolea mfano wa kazi
nzuri waliofanya kwenye swala la Jamhuri ya Afrika ya Kati na
Sudani Kusini. Mhe Mwigulu aliitaka Jumuiya ya Kimataifa imsaidie Rais
wa muda Mama Carthrine Samba Panza ili kuwezesha kipindi cha mpito na maridhiano kuwezesha zoezi la uchaguzi huru na wa haki.
Kuhusu
maswala ya kiuchumi mhe Mwigulu aliwakumbusha wajumbe wa bunge
hilo kuwa umebaki mwaka mmoja tu kumalizia mpango wa malengo ya
Maendeleo ya Milenia (MDG’s). Mhe Mwigulu aliitaka Jumuiya ya kimataifa
kuhakikisha kuwa mpango wa maendeleo baada ya 2015 unalenga nguzo tatu
mhimu akizitaja kuwa kijamii, kiuchumi na Mazingira.
Kuhusu
kiuchumi na Kijamii mhe Mwigulu alisema kuna umhimu sasa wa kuhakikisha
malengo yanalenga sector zinazogusa na kubadilisha maisha ya watu
wachini na masikini. ‘Tumekuwa na kipindi cha kutosha kushughulikia
uchumi mkubwa , tumefanikiwa sana, ila maeneo mengi sekta zilizokuwa
hazigusi maisha ya mtu masikini na hazitengenezi ajira kwa watu
masikini’ hivyo malengo yamekuza uchumi na kuongeza pengo kati ya watu
masikini na watu matajiri.
Ni kiu
yangu kuona agenda ya baada ya 2015 inalenga kuwainua masikini kwa
kulenga sekta zinazogusa maisha ya watu masikini na kutengeneza na
kubooresha fursa kwenye sekta zinazogusa watu wengi. Umhimu huo pia
utolewe kwenye swala la mazingira kwani mazingira yanaathiri zaidi
shughuli za mtu wa hali ya chini.
Mhe
Mwigulu alisisitiza kuwa kuna uhitaji mkubwa zaidi wa kuendeleza sekta
binfsi kwa kutengeneza sekta binfsi inayolenga ujasiliamali zaidi na
kutengeneza elimu ya kujiajri. Kwa sasa misaada mingi inalenga elimu ya
siasa na haki za binadam. “Elimu nzuri zaidi ni ya kujiajiri na
haki mhimu zaidi ni ya kuishitena maisha bora” kama tunasaidia
kuelimisha uraiani tusaidie kulimisha ujasiliamali, ubunifu wa miradi,
uendelezaji miradi, biashara na kutambua fursa. Misaada ilenge kutambua
fursa za uzalishaji, kuwekeza kwenye sekta za uzalishaji na kutambua
masoko. Mhe Mwigulu alisema, soko la Ulaya limekuwa likiathiri sana
mazao ya Afrika kwa bei kutokutabirika na bei kuyumba sana. Mafia
makubwa yanalinda wakulima wao na yanazuia mataifa madogo kulinda
wakulima wao.
Mataifa
makubwa yanalinda mazao ya wakulima wao kwa kuwahakikishia masoko lakini
yanawapambanisha na wakulima wa mataifa madogo wasiokuwa na ruzuku ya
kutosha na wanaopangiwa bei za chini kwa mazao yao. Tukiamua kuinua
maisha ya mkulima masikini wa Afrika, tufute wimbo wa kushuka kwa bei za
mazao yake ktk soko la Dunia huku wakulima wa mataifa makubwa wakiwa
wamepata hifadhi.
Post a Comment