NDEGE ya shirika la Ndege la Malaysia aina ya Boeing 777 iliyotoweka jana asubuhi bado haijapatikana mpaka sasa.
Ndege
hiyo iliyokuwa imebeba abiria 227 na wafanyakazi 12 kutoka nchi
mbalimbali ilipoteza mawasiliano saa moja baada ya kupaa kutoka Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Kuala Lumpur, Malaysia ikielekea Beijing,
China.
Taarifa
zinadai ndege hiyo ilianguka katika bahari karibu na visiwa vya Phu
Quoc, Vietnam. Zoezi la kutafuta ndege hiyo bado linaendelea katika
visiwa hivyo
Post a Comment