Katibu
Mkuu Utumishi Bw. George D. Yambesi akimsikiliza Mwakilishi Mkazi wa
JICA Tanzania Bw. Yasunori Onishi (kulia) akielezea kuhusu watalaam wa
kujitolea kutoka nchini Japan walivyofanya kazi hapa nchini katika
hafla fupi ya kuwaaga wataalamu hao iliyofanyika ukumbi wa Utumishi
mapema leo. Mtaalamu
wa Kujitolea katika fani ya Sayansi na Hesabu kutoka Japan Bw.
Tomotaka Tani akiwasilisha mada kuhusu uzoefu wake hapa nchini, katika
hafla fupi ya kuwaaga wataalamu sita waliomaliza muda wao hapa nchini
iliyofanyika ukumbi wa Utumishi mapema leo.
Katibu
Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi (kushoto) akitoa zawadi kwa Mtaalamu
wa kujitolea katika fani ya Sayansi na Hesabu kutoka Japan Bw. Jun
Tsuda (katikati) wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalamu sita wa
kujitolea kutoka nchini Japani iliyofanyika ukumbi wa Utumishi mapema
leo.Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa JICA Tanzanian Bw. Yasunori Onishi.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D.
Yambesi (kulia) akitoa ufafanuzi wa maswali kutoka kwa waandishi wa
habari baada ya hafla fupi ya kuwaaga wataalamu wa kujitolea kutoka
nchini Japan iliyofanyika ukumbi wa Utumishi mapema leo. Wengine ni
baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Post a Comment