
Ziara
ya Mwenyekiti wa Vijana Wilaya ya Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro Komredi
Japhar Mghamba akiongozana na Katibu Msaidizi wa Mkoa Maalum wa Vyuo
Vikuu Komredi Daniel Zenda inaendelea kwa mafanikio makubwa katika
wilaya hiyo ambapo mpaka sasa imefanikiwa kuingiza Vijana 1800 katika
Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) pamoja na
Chama.
Ziara hiyo iliyobeba
jina la Operation Kokoro iliyoanza wiki iliyopita ilipata misikosuko
hasa baada ya moja ya msafara wake kushambuliwa kwa risasi na watu
wasiojulikana. Operation hiyo inayolenga kuhamasisha Vijana wa Upinzani
na wasio na vyama kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhamasisha
Vijana wa CCM kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi ujao wa
Serikali za mitaa hapo baadae October mwaka huu pamoja na kukagua,
kuhamasisha na kuelezea katika matawi na kata juu ya utekelezaji wa
Ilani ya chama kwa kauli mbiu "CCM Mwanga Ukimya sasa Basi"
Operation kokoro
tayari imeshapita katika kata ya Kisangara, na kuendelea katika milima
ya upareni maeneo ya Ugweno, Msangeni, Kifula, Mamba na Kikweni.
Viongozi hao wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wametembelea vikundi
mbalimbali vya bodaboda, makundi ya wajasiriamali wadogo na wakubwa
pamoja na kukagua miradi iliyoainishwa kwenye Ilani ya Chama ambayo
inayoendelea kutekelezwa wilayani humo na Serikali ya Chama Cha
Mapinduzi.
Viongozi hao wakiwa
wanahutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Msangeni wamesema kuwa
wananchi waendelee kuiamini CCM kwani ndio Chama Bora Cha siasa ambacho
kinasikiliza kero za wananchi wake na kuzitafutia ufumbuzi na kutaja
kero mbalimbali ambazo tayari zimepatiwa ufumbuzi wa kudumu wilayani
humo.
Ziara hiyo inaendelea katika kata na maeneo mengine ya wilaya ya Mwanga.
Mkao wa picha.....
Picha ya pamoja....






Post a Comment