"Ni vyema
tukatambua kuwa Watanzania ni wapenda amani, hivyo wasingependa kuona
kukijitokeza tofauti kati ya wajumbe wa Bunge hilo.
Dar es
Salaam. Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Dar es Salaam,
Mwadhama Kardinal Pengo amesema shughuli za mchakato wa Katiba zifanyike
kwa amani na kwamba ziwalinde Watanzania katika umoja na mshikamano
waliyokuwa nao.
Pia,
amewataka wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kuweka masilahi yao kando na
kutanguliza masilahi ya taifa kwa faida ya Watanzania.
Akizungumza
jana kwenye uzinduzi wa Katisa Katoliki Magomeni, Kardnali Pendo
alisema ni vyema viongozi wakafahamu kwamba Watanzania ni watu
wanaopenda amani, na kwamba yeye angepAenda kuona amani iliyopo inadumu.
Alisema: "Niseme kwamba, shughuli za mchakato wa kuandika Katiba Mpya zifanyike kwa amani."
Aliongeza:
"Ni vyema tukatambua kuwa Watanzania ni wapenda amani, hivyo
wasingependa kuona kukijitokeza tofauti kati ya wajumbe wa Bunge hilo,"
Alisema
kama tunataka nia ni kupata katiba bora, ni lazima wajumbe wabunge la
Maalum la Katiba kuweka masilahi ya yao kando na kuangalia yale ya taifa
kwa faida ya Watanzania wote.
Alitoa
mfano kwa baadhi ya vingozi wa nje ya nchi wanavyotambua mchango wa Baba
wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa kuwa ni mtu aliyependa amani,
umoja na mshikamamno.
Alisema
leo (jana) alifuatilia vyombo vya habari na kusikia kuwa Rais wa
Zimbabwe (Robert Mugabe) akimuelezea Mwalimu Nyerere kama kiongozi
shupavu aliyeweka misingi ya amani Tanzania kwa kuwa alikuwa mpenda
amani.
Naye,
Paroko wa Kanisa hilo Joseph Matumaini alisema Kanisa hilo limejengwa
kwa ghalama ya Sh1.25 bilioni fedha ambazo zimetokana na michango ya
waumini wao.
Alisema:
"Kanisa hili limejengwa kwa jitihada za waumi kwa kujitolea, na kwamba
tunawashukuru wote kwa kuijenga nyumba ya mungu,"
Alisema Kanisa hilo lina uwezo wa kuchukua waumini 1500.
Chanzo, mwananchi.
Post a Comment