Mshambuliaji wa timu ya Simba Ramadhan Singano (kulia) akiwania mpira na kipa wa Ruvu Shooting, Abdallah
Rashid, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye
Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo. Katika mchezo huo Simba wameibuka na
ushindi wa mabao 3-2.
Beki
wa timu ya Simba Issa Rashid (katikati) akiwania mpira na mabeki wa
timu ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa
kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Winga
wa Simba, Haruna Chanongo (kulia) akiwania mpira na beki wa Ruvu
Shooting katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye
Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mshambuliaji
wa Simba Amri Kiemba, akijaribu kufunga bao katika mchezo wa Ligi kuu
Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mashabiki wa Simba wakishangilia moja ya bao la simba.
Kocha Mkuu wa Simba Logarusic, akiwaelekeza wachezaji wake kama ilivyokawaida yake.
Post a Comment