Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Posho juu Bungeni

 

Posho juu bungeniWAKATI Ikulu ikitangaza kuwa posho kwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba haijaongezeka, Tanzania Daima imebaini kuwa imeongezeka kwa sh 140,000 kwa siku za Jumamosi na Jumapili tofauti na ilivyokuwa siku za nyuma.
Kuongezeka kwa posho hiyo ingawa kihesabu imebaki vilevile sh 300,000 kwa siku kunatokana na Ikulu kubariki pendekezo la uongozi wa Bunge Maalum la Katiba kutaka posho ya kujikimu ambayo ilikuwa sh 80,000 iwe posho ya kikao na ile ya kazi maalumu ya sh 220,000 iwe posho ya kujikimu.
Kabla ya mageuzi hayo, siku za Jumamosi na Jumapili wajumbe walikuwa wakilipwa sh 80,000 kama posho ya kujikimu, lakini kuanzia sasa watalipwa sh 220,000 ambayo imegeuzwa kuwa posho ya kujikimu na ile 80,000 iliyokuwa ya kujikimu imegeuzwa kuwa ya kikao.


TANZANIA DAIMA
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top