Na Mwandishi Wetu, Monduli
RAIS
wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa
kuwa Mgeni Rasmi katika msimu wa pili wa mbio za Sokoine zitakazofanyika
katika Kijiji cha Monduli Juu, wilaya ya Monduli, mkoani Manyara, kama
sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 30 ya kifo cha aliyekuwa
Waziri mkuu wa Tanzania, hayati Edward Moringe Sokoine.
Rais
Kikwete anatarajiwa kuwasili wilayani Monduli ambapo pia atahudhuria
ibada maalum ya kumbukumbu itakayofanyika katioka kanisa la Monduli Juu
na baadae kushuhudia mbio zitakazofanyika katika uwanja wa shule ya
msingi Monduli Juu.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari, Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday alisema
maandalizi yam bio hizo zitakazofanyika April 12, tayari yameshaanza na
kuongeza kuwa kila kitu kinakwenbda sawa kama ilivyokuwa imepangwa.
“Mgeni
Rasmi mwaka huu ni Rais Kikwete, tumeshafanya mawasiliano yote na
tunaamini mwaka mbio zitafana na kubeba sura ya Utaifa, mwaka jana
tulimwalika Rais lakini kutokana na majukumu alishindwa kuhudhuria,
lengo letu ni kuhamasisha umoja na uzalendo na sio njaa,” alisema
Gidabuda.
Gidabuday
alisema yake imeamua kumwalika kiongozi huyo mkuu wan chi kutokana na
Heshimaaliyonayo Marehemu Sokoine katika historia ya Taifa hili na
kuongeza kuwa lengo la kuandaa mbio hizo kama ilivyokuwa mwakja jana ni
kumbapo pia kutakuwa na watu na viongozi mbalimbali.
Gidabuday
alisema kutokana na changamoto zilizojitokeza mwaka jana, kamati8 yake
imejipanga vyema kuhakikisha mbio hizo zinakuwa moja ya mashindano
makubwa yanayoandaliwa katika ardhi ya Tanzania ukiacha mbio za
Kilimanjaro Marathon zilizofanyika hivi karibuni mjini Moshi.
“Tumejiweka
sawa, mbio za mwaka jana zilituachia mengi ya kujifunza na kwa mwaka
huu tunaamini tumejifunza na tuko tayari kuwapa Watanzania burudani ya
kweli, niseme tu kwamba mwaka huu tumelenga kufanya mabadiliko makubwa
sana ukianza na zawadi kwa washindi,” alisema Gidabuday.
Aidha
Gidabuday alisema zaidi ya wanariadha pamoja na watu mbalimbali
mashuhuri wakiwemo wabunge na Viongozi mbalimbali wakuu wa nchi tayari
wameshajitokeza na kuthibitisha kushiriki mbio hizi ambazo lenge lake ni
kuhamasisha uzalendo na mshikamano.
Baadhi
ya waliomba mpaka sasa ni wanafuzni wapatao 200 kutoka katika shule za
msingi na Secondari katika maeneo ya jirani na Kijiji cha Monduli Juu
mbio zitakapofanyikia, wanariadha wazoefu akiwemo mshindiu wa mwaka jana
kilomita 21, Dickson Marwa kutoka Klabu ya Riadha ya Holili, Holili
Youth Athletic Club (HYAC).
Gidabuday
aliwataja wengine kuwa ni pamoja na watu wazima ambao mpaka sasa
wameshafikia 50 ambapo kwa mwako huu jumla ya washiriki zaidi ya 1000
wanatarajiwa kushiriki.
Post a Comment