Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tunalaani vikali fujo na uhabirifu wa
mali unaofanywa na washabiki viwanjani wakati mechi mbalimbali zikiwemo
zile za kimataifa na ligi za hapa nchini.
Tunaiomba
radhi Serikali kwa uharibifu wa viti uliotokea kwenye mechi ya Ligi ya
Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na Al Ahly ya Misri
iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Uharibifu
huo wa viti umesababisha hasara ya sh. milioni 15 kwa wamiliki wa
uwanja huo ambao ni Serikali. TFF tutalipa fedha hizo kwa Serikali
kutokana na uharibifu huo.
Tunaendelea
kuchunguza tukio hilo, huku tukijiandaa kutoa adhabu kwa klabu na
washabiki husika kulingana na kanuni zetu. Adhabu itakuwa kali ili iwe
fundisho kwa wengine.
Kwa
mujibu wa Serikali, viti kumi viling’olewa na kutupwa ovyo ovyo
uwanjani wakati vingine 40 viliathirika kutokana na vurugu za watazamaji
hao.
Tumebeba
dhamana ya kulipa uharibifu huo kwa vile TFF ndiyo wenye dhamana ya
kusimamia mechi za kimataifa, na ndiyo tulioomba idhidi ya kutumia
uwanja huo.
Kwa
vile sasa baadhi ya washabiki, wapenzi na wanachama wa klabu mbalimbali
nchini wanataka kufanya suala la uharibifu kuwa la kawaida na mazoea,
Serikali inakusudia kuchukua mapato yote ya mchezo husika endapo
kutatokea uharibifu.
Pia
kuruhusu uwanja kutumiwa bila watazamaji kwa baadhi ya mechi, na
kutoruhusu uwanja huo kutotumika kabisa kwa baadhi ya mechi.
Post a Comment