Semina
ya siku mbili kwa waamuzi wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA) na wale wa ngazi ya juu nchini (elite) kwa robo ya
kwanza ya mwaka huu inaanza kesho (Machi 15 mwaka huu) kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Waamuzi
na waamuzi wasaidizi 22 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wanashiriki
katika semina hiyo ambayo pia itahusisha mtihani wa utimamu wa mwili
(physical fitness test), na itamalizika keshokutwa (Machi 16 mwaka huu).
Baadhi
ya waamuzi hao ni Charles Simon kutoka Dodoma, Dalila Jafari
(Zanzibar), Ferdinand Chacha (Mwanza), Hamis Chang’walu (Dar es Salaam),
Helen Mduma (Dar es Salaam), Israel Mujuni (Dar es Salaam), Issa Vuai
(Zanzibar), Janeth Balama (Iringa) na Jesse Erasmo (Morogoro).
John
Kanyenye (Mbeya), Jonesia Rukyaa (Bukoba), Josephat Bulali (Zanzibar),
Lulu Mushi (Dar es Salaam), Martin Saanya (Morogoro), Mfaume Nassoro
(Zanzibar), Mohamed Mkono (Tanga), Mwanahija Makame (Zanzibar), Ngaza
Kinduli (Zanzibar), Ramadhan Ibada (Zanzibar) na Waziri Sheha
(Zanzibar).
WATANZANIA WATANO WAKWAA UKAMISHNA CAF
Watanzania
watano wameteuliwa kuingia kwenye jopo la makamishna watakaosimamia
mechi mbalimbali za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa mwaka
2014 hadi 2016.
Post a Comment