“PRESS RELEASE” TAREHE 09.03.2014.
- MWANAMUME MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA UKWAVILA AUAWA KATIKA UGOMVI.
- MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGOGWA NA GARI WILAYANI RUNGWE.
- MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA MITATU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KATIKA CHOO.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
MWANAMUME MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA UKWAVILA AUAWA KATIKA UGOMVI.
MWANAMUME
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA MPOSOLE (35) MKAZI WA MUHONGOLE
ALIUAWA KWA KUCHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI NA MAKALI SEHEMU ZA
KICHWANI NA SHINGONI NA MTUHUMIWA AITWAYE VENANCE MUYINGA UMRI KATI YA
MIAKA 30-35, MKAZI WA UKWAVILA. TUKIO HILO LILITOKEA MAJIRA YA SAA
00:01HRS USIKU WA KUAMKIA TAREHE 08.03.2014 HUKO KATIKA KIJIJI CHA
UKWAVILA, KATA YA MUHONGOLE, TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI. CHANZO
CHA MAUAJI HAYO NI UGOMVI ULIOTOKANA NA TUHUMA ZA WIZI WA BAISKELI KATI
YA MAREHEMU NA MTUHUMIWA TANGU MWAKA 2013. MTUHUMIWA ALITOROKA MARA
BAADA YA TUKIO HILO, JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI
KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAO
WAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA VYOMBO HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA
KISHERIA.
MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGOGWA NA GARI WILAYANI RUNGWE.
MWANAFUNZI
WA SHULE YA MSINGI MPUMBULI DARASA LA TANO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA
THOMAS PHILIPO (13) MKAZI WA MPUMBULI AMEFARIKI DUNIA WAKATI AKIPATIWA
MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA WILAYA MAKANDANA – TUKUYU BAADA YA KUGOGWA
NA GARI LISILOFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI WALA DEREVA WAKE. TUKIO
HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 08.03.2014 MAJIRA YA SAA 20:00HRS USIKU HUKO
KATIKA KIJIJI CHA MPUMBULI, KATA YA MPUGUSO, TARAFA YA PAKATI, BARABARA
YA TUKUYU/KYELA WILAYA YA RUNGWE. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
HOSPITALINI HAPO. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA, DEREVA ALIKIMBIA MARA
BAADA YA AJALI HIYO NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO
KWA KUZINGATIA/KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA
AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. PIA ANATOA WITO KWA WATUMIAJI WENGINE WA
BARABARA KUWA MAKINI WATUMIAPO BARABARA IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI IKIWA NI PAMOJA NA KUVUKA KATIKA
ALAMA ZA KUVUKIA [ZEBRA CROSSING]. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE
TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA MITATU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KATIKA CHOO.
MTOTO
MWENYE UMRI WA MIAKA MITATU (03) ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA INNOCENT
OSCAR MKAZI WA KIJIJI CHA ILUNDO AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA
KATIKA SHIMO LA CHOO KILICHOKUWA KIMEJAA MAJI. TUKIO HILO LIMETOKEA
MNAMO TAREHE 08.03.2014 MAJIRA YA SAA 15:00HRS ALASIRI HUKO KATIKA
KIJIJI CHA ILUNDO, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE.
CHANZO CHA KIFO CHA MTOTO HUYO NI BAADA YA KWENDA KUJISAIDIA KATIKA
CHOO HICHO AKIWA PEKE YAKE. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI KWA KUWEKA UANGALIZI WA KUTOSHA KWA WATOTO WAO
ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA. PIA ANATOA WITO KWA WAMILIKI
WA NYUMBA KUWA NA KAWAIDA YA KUANGALIA UIMARA WA VYOO HASA VYA SHIMO
ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUTOKEA KAMA HAYO. AIDHA ANATOA WITO KWA
JAMII KUFUKIA MASHIMO AMBAYO HAYATUMIKI NA KUFUNIKA VISIMA VILIVYOPO
KATIKA MAENEO YAO KWANI NI HATARI KWA WATOTO UKIZINGATIA TUNAELEKEA
KATIKA KIPINDI CHA MVUA NYINGI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA BESTA HASSAN (48) MKAZI WA KYIMO AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI
[GONGO] UJAZO WA LITA 20 KATIKA NDOO YA PLASTIC. MTUHUMIWA ALIKAMATWA
KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 08.03.2014 MAJIRA YA SAA 13:00HRS
MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA KYIMO, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA
RUNGWE. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTENGENEZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZA
KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA
NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment