Bi. Jacqueline Mkindi akisisitiza Jambo wakati wa hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
Na. Mwandishi Wetu
KATIKA
kuhakikisha kwamba thamani ya mazao ya horticulture(maua, na mboga
mboga) nchini Tanzania inapanda na hivyo kupata masoko ya uhakika ndani
na nje ya nchi, Tanzania Horticultural Association
(TAHA),
imeamua kuendeleza harakati hiyo kwa kutoa mafunzo ya misingi bora ya
kilimo kwa mazao hayo kwa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Mafunzo
hayo ya siku tatu yaliyofanyika hivi karibuni wilayani Makete ambayo
yanalenga kutoa misingi fasaha na mbinu zinazotumia teknolojia rahisi za
kisasa ili kuongeza tija na thamani kwenye mazao ya horticulture
yamezinduliwa hivi karibuni na Mkurugenzi wa SUMA JKT, Brigedia Jenerali
Mwanamakala Mohamed Killo, sambamba na Mkurugenzi Mtendaji wa TAHA, Bi.
Jacqueline Mkindi.
Aidha,
mafunzo hayo yanayoendeshwa na mtaalamu wa kilimo cha mazao ya
horticulture wa TAHA, Manfred Bitala, katika ukumbi wa klabu ya jeshi la
JKT Ruvu, yanafanyika kwa nadharia na vitendo ambapo maafisa wa Jeshi
waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo hayo watajifunza kwa vitendo mbinu
hizo kwenye moja ya mashamba yaliyo katika eneo la jeshi hilo.
Mkurugenzi wa SUMA JKT, Brigedia Jenerali Mwanamakala Mohamed Killo akizungumza na washiriki wa mafunzo.
Awali
alipokuwa akifungua mafunzo hayo siku ya Jumatatu Mkurugenzi wa SUMA
JKT, Brigedia Jenerali Killo, alisema kuwa mafunzo hayo yatasaidia
kuleta mapinduzi ya kilmo bora cha mazao ya horticulture yenye kukidhi
viwango vyenye ubora wa kimataifa na hivyo kuvutia soko na uwekezaji
kwenye sekta hiyo nchini.
“Uzoefu
wa masuala ya msingi ambayo wataalamu wa Jeshi letu wataupata utakuwa
chachu ya kuleta mapinduzi ya kilimo bora cha mazao ya horticulture
yenye kukidhi viwango vya ubora wa kimataifa na hivyo kuvutia wawekezaji
na soko nchini,” alisisitiza Brigedia Killo.
Akizungumza
wakati wa hotuba yake ya ufunguzi, Mkurugenzi Mtendaji wa TAHA, Bi.
Jacqueline Mkindi, alibainisha kuwa licha ya Jeshi hilo kupata
mafanikio katika kuzalisha maelfu ya tani za mazao ya horticulture kila
mwaka, jitahida zaidi za jeshi hilo zinahitajika ili kuongeza viwango
vya uzalishaji vinavyokidhi masoko ya kimataifa kila mwaka.
Mkurugenzi
wa SUMA JKT, Brigedia Jenerali Mwanamakala Mohamed Killo akifurahia
jambo wakati alipokuwa akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo hayo
katika ukumbi wa JKT CLUB RUVU.
Bi.Mkindi,
aliongeza kuwa Tanzania inayo fursa nyingi za uzalishaji na uwekezaji
katika sekta ya mazao ya horticulture ingawa fursa hizo zinaendelea
kubaki wazi hadi sasa pasipo kutumiwa ipasavyo.
Mkurugenzi
huyo wa TAHA, ameto wito kwa jeshi hilo kupitia mafunzo wanayoyapata
kuwa mfano kwa kuzitumia fursa za uwekezaji na masoko ya mazao ya
horticulture nchini.
Katika
kipindi cha mwaka uliopita Jeshi la JKT-Ruvu lilizalisha mzao
mbalimbali kwenye shamba la majaribio ikiwemo; kilo 22,797 za (mchicha),
kilogramu 24,175, (nyanya), kilogramu 31,438 (matango) ni kilogramu
12410 (bilinganya) na Vitunguu kilo 2211.
Ndugu
Manfred Bitala mtaalamu wa ufundi wa kilimo cha mazao ya horticulture
wa TAHA akitoa mwongozo wa mafunzo ya kilimo cha mazao ya horticulture.
Washiriki wa mafunzo wakimsikiliza Mkurugenzi wa SUMA JKT, Brigedia Jenerali Mwanamakala Mohamed Killo.
Mkurugenzi
wa TAHA katika picha ya pamoja na maafisa wa Jeshi la JKT wanaohudhuria
mafunzo ya uzalishaji wa mazao ya horticulture yenye tija na thamani.
Post a Comment