Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Pro. Elisante Ole
Gabriel akifungua Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi,
Taharabu, Kizazi Kipya na Utenzi siku ya Jumamosi katika Viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi katika Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi,
Taharabu, Kizazi Kipya na Utenzi Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
Bi. Regina Kikuli akitoa hotuba fupi wakati wa tamasha hilo, kulia ni
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Pro. Elisante
Ole Gabriel.
Mshereheshaji
kutoka kikundi cha Temeke akionyesha umahiri wake kwa kula moto wakati
wa Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi, Taharabu, Kizazi
Kipya na Utenzi lililofanyika siku ya Jumamosi katika Viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar es Salaam.
Kundi
la muziki wa dansi lijulikanalo kwa jina la Mashujaa wakitumbuiza
wakati wa Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi, Taharabu,
Kizazi Kipya na Utenzi siku ya Jumamosi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam.
Viongozi
wa makundi ya muziki wa Dansi, Taharabu, Kizazi kipya na Utenzi
waliooshiriki katika Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi,
Taharabu, Kizazi Kipya na Utenzi wakiwa katika picha ya pamoja ambapo
katika mziki wa dansi kundi la Msondo ngoma liliibuka kidedea huku
upande wa taharabu Jahazi Modern Taharabu walishika nafasi ya kwanza
huku muziki wa kizazi kipya msanii Kelvini Nyoni kuwabwaga wenzake na
katika fani ya Utenzi Bi. Mariam Mponda kushika nafasi ya kwanza.
Picha na Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini WHVUM
Post a Comment