Na Magreth Kinabo –MAELEZO, Dodoma.
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba, Anne Makinda ametoa changamoto kwa wajumbe
wenzake wanawake walio kwenye Bunge hilo, kujenga hoja zenye nguvu
zinazohusu masuala yanayohusu wanawake na kuzitetea kwa sauti moja ili
ziweze kupita katika Rasimu ya Katiba.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Mhe. Anne ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania wakati akitoa mchango wake kwa wajumbe wa
semina ya kujenga agenda muhimu kwa masuala ya kijinsia iliyoandaliwa na
Umoja wa Wabunge Wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
(TWPG) kwa wajumbe wanawake wa Bunge hilo, iliyofanyika kwenye Ukumbi
wa Pius Msekwa.
“
Ninawaomba tuwe na hoja zenye nguvu wakati wakuchangia mjdala wa Rasimu
ya Katiba . Tukisimama kwa hoja za nguvu na kutetea vifungu
vinavyohusu masuala ya wanawake tunaweza kubadilisha vifungu.
Tuzungumzeni hoja tuache kufanya fujo, tusiingie katika malumbano ambayo
hayana tija, tuache kuzomea tukifanya hiyo tutakuwa tumejijengea
heshima,” alisema Mama Anne.
Kwa upande
wake mmoja wa mtoa mada katika semina hiyo,kuhusu haki za wanawake,
utu, hali ya maisha na mgawanyo wa rasilimali, Ussu Mallya, ambaye pia
ni wanaharakati wa masuala ya wanawake aliwataka wajumbe hao
,wanawake kutetea saula la Usawa wa Kijinsia liingizwe katika Rasimu
ya Katiba likiwa ni moja ya Tunu za Taifa.
Mtoa
mada mwingine ambaye pia mjumbe Bunge hilo na ni Makamu Mwenyekiti wa
TWPG, Suzan Lyimo alisema ni vema wanawake hao kupigania asiliamia 50
inakuwepo ili kuhakikisha masuala yote yanayohusu wakina mama yakuwemo,
mfano kwenye nafasi za ubunge, ajira na ngazi zingine za maamuzi.
Suzan alisema hayo wakati akitoa mada kuhusu Uwakilishi wa wanawake, katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mada
nyingine iliyotolewa katika semina hiyo ni masuala ya miradhi na
ndoa iliyotolewa na Victoria Mandari kutoka Chama cha Wanasheria
Wanawake Tanzania(TAWLA) ambaye aliwataka wajumbe hao kutoendeleza
mambo ya mila na desturi ambayo yanamkandamiza mwanamke.
Katika semina hiyo, baadhi ya
wanawake hao walipendekeza masuala ya haki ya elimu kwa wanawake, haki
za uzazi salama, haki ya kumiliki mali, haki ya ulinzi kwa wanawake na
watoto, haki ya mtoto wa nje ya ndoa, umri wa mtoto kuolewa kuwa ni
miaka 18 kuingia katika rasimu hiyo.
Post a Comment