Mwenyekiti wa
Wabunge wanawake Anna Abdallah (kulia) akifungua semina ya Wabunge
wanawake wa Bunge Maalum la Katiba leo mjini Dodoma uliokuwa
ukijadiliana juu ya umuhimu wa kuwekwa kwa umri wa mtoto katika Katiba
mpya na umri unatakiwa kuolewa na kuoa na masuala ya uzazi
salama. Kushoto ni NaibuWaziri wa Katiba na Sheria Mhe Angelah Kairuki.
Mjumbe
wa Bunge la Katiba ambaye pia Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia
na Watoto Dkt Pindi Chana akitoa maoni yake leo mjini Dodoma wakati wa
semina ya Wabunge wanawake wa Bunge Maalum la Katiba uliondaliwa na
Chama cha Waandishi wanawake Tanzania (TAMWA) juu ya kuwaelimisha
masuala mbalimbali ya kuzingatia wakati wa utungaji wa Katiba mpya
ikiwemo uzazi salama na kutoa ufafanuzijuu ya umri wa mtoto.Mjumbe wa Bunge la Katiba ambaye pia Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimuakitoa
maoni yake leo mjini Dodoma wakati wa Mkutano wa Wabunge wanawake wa
Bunge Maalum la Katiba uliondaliwa na Chama cha Waandishi wanawake
Tanzania (TAMWA) juu ya kuwaelimisha masuala mbalimbali ya kuzingatia
wakati wa utungaji wa Katiba mpya ikiwemo uzazi salama na kutoa
ufafanuzijuu ya umri wa mtoto.
Baadhi
ya wanawake ambao ni Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wakifuatilia
mada mbalimbali zilikuwa zinawaelimisha juu ya umuhimu wa kuzingatia
masuala ya usawa wa kijinsia , haki za uzazi salama wakati wa kuandika
Katiba mpya. Semina hiyo ambayo imefanyika leo mjini Dodoma
imeandaliwa na TAMWA.
Picha na MAELEZO_ Dodoma.
Post a Comment