“PRESS RELEASE” TAREHE 22.03.2014
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA MINNE AFARIKI DUNIA AKIWA ANAOGELEA KATIKA MTO NZOVWE.
MTOTO
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ALBERT LAZARO MWENYE UMRI WA MIAKA MINNE,
MKAZI WA ISONDA ITENDE AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUFA MAJI NA MWILI WAKE
UMEKUTWA UKIELEA KATIKA MTO NZOVWE ULIO JIRANI NA NYUMBA YAO.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 21.03.2014 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI HUKO
MBALIZI, TARAFA YA USONGWE MBEYA VIJIJINI. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. UCHUNGUZI NA UPELELEZI WA
TUKIO HILO UNAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI NA JAMII KWA UJUMLA KUWA MAKINI NA
WATOTO WAO IKIWA NI PAMOJA NA KUWAKATAZA KWENDA KUOGELEA AU KUCHEZA
KARIBU NA MITO/MABWAWA/MADIBWI YALIYOKO KARIBU NA MAENEO YAO KWANI NI
HATARI HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA. AIDHA
ANATOA WITO KWA JAMII KUFUKIA/KUFUNIKA VISIMA NA MADIBWI YALIYOKO KATIKA
MAENEO YAO KWANI NI HATARI KWA WATOTO.
NYUMBA YENYE VYUMBA VIWILI YATEKETEA KWA MOTO JIJI MBEYA.
NYUMBA
MOJA YENYE VYUMBA VIWILI MALI YA FRANCIS SAMSON (31) MKAZI WA INYALA
JIJI MBEYA YATEKETEA KWA MOTO PAMOJA NA MALI ZOTE ZILIZOKUA NDANI YA
NYUMBA HIYO.
TUKIO
HILO LA MOTO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 20.03.2014 MAJIRA YA SAA 12:45
MCHANA HUKO MTAA WA INYALA, KATA NA TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA
MBEYA.
KATIKA
TUKIO HILO MALI ZOTE ZILIZOKUWEMO NDANI YA NYUMBA HIYO ZILITEKETEA KWA
MOTO IKIWA NI PAMOJA NA GODORO, KITANDA NA VYOMBO MBALIMBALI AMBAVYO
THAMANI YAKE BADO HAIJAFAHAMIKA.
CHANZO
CHA MOTO HUO BADO HAKIJAFAHAMIKA. HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU
YALIYORIPOTIWA KUTOKEA. MOTO ULIZIMWA KWA JITIHADA ZA WANANCHI, KIKOSI
CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI PAMOJA NA JESHI LA POLISI. UCHUNGUZI ZAIDI WA
TUKIO HILO UNAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO JAMII KUCHUKUA
TAHADHARI NA MATUKIO YATOKANAYO NA MOTO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI:
KATIKA
MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KATIKA KIJIJI CHA NDANDALO, KATA YA KYELA-KATI,
TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA TAREHE 21.03.2014 MAJIRA YA SAA
11:00 ASUBUHI MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SADICK JULIUS (29)
MKAZI WA KIJIJI CHA NDANDALO ALIKAMATWA AKIWA NA POMBE KALI [VIROBA]
ILIYOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI AINA YA RIDDER KATONI MOJA [01].
MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIZO, TARATIBU ZA KISHERIA ZINAENDELEA NA MARA ZITAKAPO KAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA KUACHA MARA MOJA KUJIHUSISHA NA
BIASHARA YA UUZAJI NA USAMBAZAJI WA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA
SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA PIA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
KATIKA
MSAKO MWINGINE ULIOFANYIKA HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA
MAFYEKO,TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA TAREHE 20.03.2014 MAJIRA
YA SAA 10:30 ASUBUHI MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SAULO
ZEPHANIA (48) MKAZI WA KIJIJI CHA MAFYEKO ALIKAMATWA AKIWA
AMELIMA/AMEPANDA ZAO HARAMU LA BHANGI MICHE 12 YENYE UREFU FUTI 2.5
KWENYE SHAMBA LAKE LA MAHINDI.
MTUHUMIWA NI MKULIMA WA ZAO HILO HARAMU, TARATIBU ZA KISHERIA ZINAENDELEA NA MARA ZITAKAPO KAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MARA MOJA KULIMA ZAO HARAMU LA
BHANGI WALA KUUZA/KUSAMBAZA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA
AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA KWA
JESHI LA POLISI ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA ULIMAJI/UUZAJI NA
USAMBAZAJI WA BHANGI ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE
DHIDI YAO.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment