Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akifungua mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na
Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo
Machi 17, 2014. Picha na OMR
…………………………………….
Na Frank Shija – WHVUM
Imeelezwa kuwa Tanzania ni nchi ambayo ina ardhi kubwa na yenye rutuba amaboya haijatumiwa kwa shughuli za kilimo na uzalishaji.
Hayo
yamebainishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Gharib
Bilal wakati akifungua kongamano la Kibiashara Baina ya Tanzania na
Israel lililoanza leo jijini Dar es Salaam.
Dkt.
Bilal amesema kuwa Tanzania ina jumla ya hekta milioni 44 ambazo ni
nzuri na zenyerutuba na kuongeza kuwa kati ya hizo jumla ya hekta
milioni 29 zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji.
“Ndugu
mwenyekiti katika hekta milioni 44 zilizopo, zaidi ya hekta milioni 29
zinafaa kwa matumizi ya kilimo cha umwagiliaji,hivyo ni fursa kwa
wawekezaji kutoka Israel kushirikiana na wananchi wa Tanzania ili
kuendeleza kilimo cha kibiashara hapa nchini” Alisema Dkt. Bilal.
Aidha
Dkt Bilal ameipongeza Kampuni ya Kingdom Leadership Network Tanzania
ambao ndiyo waandaaji wa kongamano hilo na kuongeza kuwa kupitia
kongamano hilo fursa za uwekezaji katika sekta ya kilimo itazidi
kuimarika na kukuza sekta ya kilimo ikiwemo uzalishaji wa chakula cha
ziada.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Kingdom
Leadership Network Tanzania (KLNT) Ibrahim Kaduma ametoa wito kwa vijana
kuchangamkia fursa na kujishughulisha na kilimo cha kibiashara kwani
ndiyo sekta pekee unayoweza ukajiari kwa faida ya uhakika.
Kaduma
aliongeza kuwa kongamano ili lemelenga kukuza ushirikiano wa kibiashara
baina ya Tanzania na Israel hususani katika sekta ya kilimo ili
kuongeza tija na kwa taifa la Tanzania.
Wakati
huo huo baadhi ya washiriki wa kongamano hilo akiwemo Mkuu wa Maendeleo
ya Biashara na Uhusiano wa kampuni ya Balton Tanzania Bi. Linda Byaba
amesema kuwa wao wao katika kongamano ili umekuja wakati muufaka ambapo
wamezindua mpango wa kufundisha vijana juu ya kilimo cha kibiashara
unaojulikana kwa jina la “Farming is Cool Project”
Linda
amesema kuwa kupitia mpango huo vijana wengi watanufaika kwa kupata
mafunzo mbalimbali ikiwemo kilimocha kisasa, elimu ya ujasiriamali na
stadi za maisha na kuongeza wamekuwa na ushirikiano mzuri na Serikali
hivyo mpango huu utatekelezwa kwa ufanisi na kuleta tija kwa taifa.
“Kampuni
yetu imezindua mpango ambao utawanufaisha vijana wengi wa Kitanzania
katika kuwapati elimu ya ujasiriamali, kilimo na stadi za maisha, hivyo
napenda kutoa wito kwa vijana kutumia fursa hii kupata elimu tena
inatolewa bure kabisa” Alisema Linda.
Kongamano
hilo linafanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius
Nyerere ambapo utadumu kwa muda wa siku tatu hadi alhamisi, ambapo
kongamano hilo limeratibiwa na kampuni ya Kingdom Leadership Network
Tanzania(KLNT) likiwa na lengo la kukutanisha wafanyabiashara wa Israel
na Tanzania wanaojihusisha na sekta ya kilimo.
Post a Comment