Afisa
habari Mwandamizi wa Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika
utumishi wa Umma Bi Riziki Abrahamu akiwaonyesha waandishi wa habari
moja ya nakala ya maombi ya ajira isiyokidhi vigezo hali inayosababisha
waombaji wengi wenye sifa kushindwa kupata ajira Serikalini. Kulia ni
Afisa Habari Idara ya Habari Maelezo Frank Mvungi na kushoto ni Afisa
Udhibiti na Ubora wa Sekretarieti hiyo bw. Chistopher Liganga.
Afisa
habari Mwandamizi wa Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika
utumishi wa Umma Bi Riziki Abrahamu akiwaeleza waandishi wa habari leo
jijini Dar es salaam kuhusu waombaji kazi kujiandaa vyema ili kukidhi
vigezo vya usaili, na kushoto ni Afisa Udhibiti na Ubora wa
Sekretarieti hiyo bw. Chistopher Liganga.
…………………………………………………………………………
Frank Mvungi-Maelezo
Ofisi
ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kuandaa programu
ya Elimu kwa umma ili kuwawezesha waombaji wa kazi kuweza kutimiza
vigezo vinavyohitajika ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kupata kazi
walizooomba.
Hayo
yamesemwa na Afisa Habari Mkuu wa Sekretarieti ya Ajira Bi Riziki
Abraham wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es
salaam.
Akifafanua
Bi Riziki amesema mpango huo unalenga kuwajengea uwezo waombaji wa
ajira kuweza kuandaa wasifu wao vyema (CV), kuandika barua za maombi
kwa ufasaha, kuwajengea uezo wa kufanya maandalizi sahihi kabla ya
usaili.
Aliongeza
kuwa hali hiyo inatokana na kujitokeza kwa changamoto za wahitimu walio
wengi kushindwa kutimiza vigezo husika ili waweze kupata ajira
wanazoomba.
Bi
Riziki alisisitiza na kusema kuwa katika kutekeleza mpango huo
watashirikiana na Taasisi za Elimu hapa nchini ili kuwasaidia wanafunzi
wanaohitimu vyuoni ili kuwajengea uwezo ili waweze kukidhi vigezo mara
wanapoomba ajira Serikalini.
Katika
kipindi cha miaka mine Tangu kuanzishwa kwa Sekretarieti ya Ajira
katika utumishi wa umma imekabiliana na changamoto nyingi ikiwemo ubora
wa wahitimu wanaowasilisha maombi ya kazi Serikalini kuanzia ngazi ya
Sekondari, Astashahada ya juu, Shahada ya uzamili pamoja na shahada ya
uzamivu.
Pia
Bi Riziki alibainisha kuwa katika tathmini sekretarieti kupitia maombi
ya ajira yaliyowasilishwa wamebaini mapungufu yatokanayo na ubora hafifu
wa baadhi ya wahitimu wanaoomba kazi kupitia chombo hiki.
Dhana
potofu ya wahitimu kuwa kuwa na vyeti pekee ndicho kigezo pekee cha
mhitimu kupata ajira badala ya kuwa na uelewa mpana wa kile walichoombea
kazi,kutotilia maanani sifa na masharti ya Tangazo husika,
kutojiamini,kukosa uzoefu wa kazi inayohitaji uzoefu na uwezo mdogo
wakutumia lugha kwa ufasaha.
Post a Comment