Msemaji
wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bw. Richard Kasuga akiwaeleza
waandishi wa habari kuhusu tahadhari ya kutokea viwavi jeshi hapa
nchini hivyo wananchi kutakiwa kuchukua tahadhari. Kulia ni Afisa Habari
wa Idara ya habari Maelezo na kushoto ni Mkurugenzi Msidizi Afya ya
Mimea,Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bw. Fabian Nkondo. Mkurugenzi
Msaidizi Afya ya Mimea,Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bw. Fabian
Nkondo akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu hatua zinazochukuliwa na
Serikali katika kuwaelimisha wananchi kuhusu maboresho katika Sekta ya
Kilimo ili kuleta Tija.
………………………………………………………………………
Frank Mvungi-Maelezo
Serikali imewatahadharisha wakulima nchini kuhusu uwezekano wa kutokea kwa viwavi jeshi katika msimu huu wa kilimo.
Hayo
yamesemwa na Msemaji wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bw.
Richard Kasuga wakati wa mkutano na vyombo vya habari leo jijini Dar es
salaam.
Akieleza
Bw. Kasuga amesema ili kuhakikisha kuwa kazi ya kukabiliana na viwavi
jeshi inafanyika kwa umakini na ukamilifu wakulima kote nchini
wanahimizwa kukagua mashamba yao mara kwa mara ili kubaini dalili za
viwavi jeshi mapema hususani kwa mazao kama mahindi, mtama, uwele,
ulezi, mpunga, ngano na shayiri .
Akifafanua
zaidi Bw. Kasuga amesema ni vyema wakulima wanapaswa kutoa taarifa za
awali pale wanapoona dalili za kuwepo kwa viwavi jeshi kwa kuwasiliana
na Maafisa ugani na kuzingatia ushauri wa kitaalamu watakaopewa na
kuupeleka kwa wakulima ambao ni walengwa.
Aliongeza
kuwa Wakulima wamejengewa uwezo tangu 2008 ili kuweza kufanya utabiri
kwa kuwapatia mafunzo na kusambaza mitego 374 ya utabiri wa viwavijeshi
sambamba na vipima mvua katika vijiji vya mikoa ya ya Tanga,
Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Morogoro, Dodoma, Lindi, Pwani na Mtwara.
Bw.
Kasuga vilevile alisema kuwa jumla ya lita 10,400 za viatilifu vya
udhibiti wa viwavijeshi vilisambazwa katika Makao makuu ya Kanda ambapo
kanda ya Nyanda za juu Kusini (Mbeya) lita 2000, Kanda ya Magharibi
(Shinyanga) lita 1000, Kanda ya Kati (Dodoma ) lita 4,000 Kanda ya
Kaskazini (Arusha) lita 2000 na Kanda ya Mashariki Dar es salaam Lita
1,400.
Hadi
mwezi Machi 2014 mlipuko ya viwavi jeshi imetokea na kudhibitiwa katika
mikoa 9 ambayo ni Mtwara, Lindi, Pwani, Mbeya, Morogoro, Dodoma,Tanga,
Arusha, na Kilimanjaro.
Aidha
Kasuga alizitaka halmashauri za Wilaya kote nchini kufuatilia mtandao
wa mitego ya utabiri katika ngazi ya vijiji na kuwahimiza watabiri wa
vijiji husika kuendelea na kazi hiyo kwa msimu mzima wa kilimo.
Wizara
ya Kilimo Chakula na Ushirika inaendelea na kazi ya kuratibu shughuli
za kukabiliana na milipuliko ya viwavijeshi, kwelea kwelea, nzige na
panya katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Post a Comment