Siku
ya Taifa ya Kutundika Mizinga itaadhimishwa kitaifa mkoani Katavi
katika wilayani Mlele tarehe 18 Machi 2014. Aidha, siku hiyo mikoa
mingine itaadhimisha kimkoa katika wilaya na vijiji vilivyochaguliwa.
Kauli Mbiu ya mwaka huu ni: “Boresha Ufugaji Nyuki, Linda Ubora wa Mazao
Yake”.
Madhumini
ya siku hii ni kuendeleza Ufugaji Nyuki unaolenga kuongeza idadi ya
wafuga nyuki, usimamizi bora wa makundi ya nyuki na kuongeza uzalishaji
wa mazao ya nyuki kwa kuzingatia ubora na teknolojia za kisasa. Aidha,
siku hii inatumika kuhamasisha uhifadhi endelevu wa raslimali za misitu
na nyuki.
Siku hii itakuwa chachu ya kuwahamasisha wadau na wananchi kwa ujumla kushiriki kwa wingi katika ufugaji nyuki wa kisasa.
Mgeni
Rasmi atakuwa Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mb), ambaye
atashiriki kutundika mizinga katika msitu wa Mlele Kusini eneo la
Kanembela na baadaye kuhutubia wananchi.
Wizara
ya Maliasili na Utalii inatoa wito kwa wadau na wananchi kwa ujumla
kushiriki kikamilifu katika kufanikisha siku hii kwenye maeneo
yaliyopangwa na maeneo binafsi.
MAENEO YATAKAYOTUNDIKWA MIZINGA KATIKA MIKOA MBALIMBALI TANZANIA BARA
NA
|
MKOA
|
WILAYA
|
KIJIJI
|
MHUSIKA/
WAHUSIKA
|
ENEO LA KUFUGIA
|
1
|
Simiyu
|
Busega
|
Mkula
|
Kikundi cha Imarika
|
Msitu wa Kikundi na Kijiji
|
2
|
Geita
|
Geita
|
Itina
|
Kikundi cha Itina
|
Msitu wa Kijiji (Ngitiri)
|
3
|
Mwanza
|
Ilemela
|
Kasamwa
|
Kikundi
|
Ngitiri ya kijiji
|
4
|
Mara
|
Musoma
|
|
Magereza
|
Msitu wa Magereza
|
5
|
Kagera
|
Missenyi
|
Kenyana
|
Kikundi cha Shubira
|
Miti katika Mashamba
|
6
|
Ruvuma
|
Songea
|
Mtyangimbole
|
Kamati ya Usimamizi Shirikishi Misitu
|
Misitu wa Songea Fuel
|
7
|
Mtwara
|
Mtwara
|
Mnivata
|
Kikundia
|
Msitu wa Halmashauri Mtiniko Mnivata
|
8
|
Lindi
|
Ruangwa
|
Liuguru
|
Kikundi cha Ufugaji Nyuki
|
Msitu wa Kijiji Liuguru
|
9
|
Iringa
|
Iringa
|
Mgera na Mngalali
|
|
Msitu wa Ubena
|
Mufundi
|
Shamba la Miti Sao Hill
|
Shamba la Miti Sao Hill
|
Shamba la Miti Sao Hill
|
10
|
Mbeya
|
Momba
|
Chilanu na Nzoka
|
Vikundi vya Ufugaji Nyuki
|
Mlima Malinde
|
11
|
Njombe
|
Ludewa
|
Mapogoro na Mavale
|
Vikundi vya Ufugaji nyuki
|
Msitu wa Sikaranyumbo
|
12
|
Rukwa
|
Kalambo
|
Kisumba, Kafukoka
|
Vikundi vya ufugaji nyuki
|
Msitu wa mto Kalambo
|
Nkasi
|
Vijiji (5) Chala A, B, na C, Chalakima na Chatekelesha
|
Vikundi vya ufugaji nyuki kila kijiji mizinga 10
|
Msitu wa Mlima Chale
|
13
|
Tanga
|
Korogwe
|
Mkwakwani Myusi
|
Kikundi cha Ufugaji Nyuki
|
Hifadhi ya asili Amani
|
14
|
Arusha
|
Arumeru
|
Nkwenankoli
|
Kamati ya Maliasili ya Kijiji
|
Hifadhi ya Msitu wa TFS
|
15
|
Kilimanjaro
|
Moshi
|
Kahe
|
NGO
|
Msitu wa Halmashauri
|
16
|
Tabora
|
Sikonge
|
Utyatya
|
Kikundi cha Wafugaji Nyuki Nyahua
|
Bwawa la Utyatya
|
17
|
Kigoma
|
Uvinza
|
Uvinza
|
Kazaroho beekeepers cooperative society
|
Msitu wa Basanza
|
18
|
Shinyanga
|
Shinyanga
|
Ukimbagu
|
NAFRAC na Kikundi cha Wafugaji Nyuki Ugimbagu
|
Shamba la Albano Malila
|
19
|
Katavi
|
Mlele
|
Kanembela
|
Kikundi cha Ufugaji Nyuki
|
Msitu wa Mlele
|
20
|
Morogoro
|
Ulanga
|
Mselezi
|
Kikundi cha ufugaji Nyuki SEMA
|
Msitu wa Hifadhi Mselezi
|
Gairo
|
Msingisi
|
TFS – Meneja Wilaya
|
Msitu wa Hifadhi Msingisi
|
21
|
Pwani
|
Bagamoyo
|
Msinune
|
Kikundi cha Ufugaji Nyuki
|
Msitu wa Simbo
|
Mkuranga
|
Kibuyuni
|
Kamati ya Maliasili na Mazingira ya kijii
|
Msitu Masanganya
|
22
|
Dodoma
|
Kongwa
|
Nyamkonga
|
Kikundi cha Ufugaji Nyuki
|
Msitu wa Halmashauri ya Wilaya
|
23
|
Singida
|
Mkalama
|
Nkungi
|
Kikundi cha ufugaji Nyuki
|
Msitu wa Kijiji
|
24
|
Manyara
|
Babati
|
Haraa
|
Kikundi cha ufugaji Nyuki
|
Msitu wa Kijiji
|
|
Imetolewa na:
S.Gesimba
Naibu Katibu Mkuu,
Wizara ya Maliasili na Utalii,
11/03/2014
on Wednesday, March 12, 2014
Post a Comment