VIONGOZI
wa Chama kipya cha siasa cha Alliance for Change and Transparency
(ACT), juzi walijikuta wakizomewa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye Uwanja wa Shule ya Mbugani, Jimbo la Nyamagani, jijini Mwanza.
Mbali
ya kujikuta katika wakati mgumu wa kuzomewa, baada ya mkutano huo
kumalizika, viongozi hao waliondolewa chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Mkutano
huo ulilenga kukitambulisha chama hicho ambacho bado hakijapata usajili
wa kudumu. Viongozi waliokumbwa na kadhia hiyo ni Mwenyekiti wa muda wa
ACT Taifa, Bw. Lucas Limbu, Katibu Mkuu wa muda, Bw. Samson Mwigamba na
Bw. Willy Mushumbusi (Katibu wa chama hicho jijini Mwanza).
Viongozi
hao walizomewa na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), ambao walihudhuria mkutano huo baada ya viongozi hao
kukishambulia chama chao.
Mwenyekiti
wa chama hicho Wilaya ya Misungwi, mkoani humo, Jane Kajoki ambaye
mwaka 2010 aligombea ubunge jimbo hilo kwa tiketi ya CHADEMA, alisema
lengo la kuanzisha chama kipya ni kumkomboa Mtanzania maskini.
Malengo
mengine ni kusimamia haki ya kila mwananchi ambaye anapaswa kushiriki
katika maamuzi ya nchi yake na kuongeza kuwa, chama hicho kimepata
udhamini wa wanachama 200 kila Mkoa ili kiweze kupata usajili wa kudumu
ambao utakiwezesha kiweze kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Wakati
akiendelea kusalimia wananchi na kukishambulia CHADEMA, Kajoki naye a
ijikuta akizomewa na kuambiwa msaliti ambapo pamoja na kuwasihi
wananchi, wamsikilize jitihada hizo zilionekana kugonga mwamba
wakionesha alama ya vidole viwili ambayo hutumiwa na CHADEMA.
Wakati
Bw.Limbua kihutubia wananchi, alikishambulia CHADEMA na kujikuta
akizomewa na wafuasi wa chama hicho ambao walishiriki mkutano huo.
Bw.Limbu
aliwafananisha wafuasi wa chama hicho sawa na mbwa waliotumwa kwenda
kuwazomea ambapo hali ya kuzomea, pia ilimkuta Bw. Mwigamba ambapo
wakati akihutubia, wafuasi hao walionesha alama ya vidole viwili kila
alipoeleza udhaifu wa viongozi wa CHADEMA na kukiponda chama hicho.
Wakiwa
jukwaani kwa nyakati tofauti, Bw.Limbu na Bw.Mwigamba, walionekana
kuchochea hasira za wafuasi hao baada ya kuifananisha CHADEMA na CCM
sawa na nguruwe pori.
Bw.
Mwigamba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, mkoani Arusha, alisema
chama hicho kikichukua nchi, kitaongoza kidikteta na kuongeza kuwa;
"Mliotumwa kuja kuzomea mnabweka kama mbwa, kwa vile mnatuzomea, nasi
tunajiandaa kuwazomea viongozi wenu mahali popote," alisema Bw.Mwigamba.
Alisema
baadhi ya vyama vimeanzishwa na kuendeshwa kama kampuni za watubinafsi,
kufukuza watu kabla hakijashika madaraka sasa kikichukua nchi hali
itakuwaje.
Aliwaomba
wananchi kukiunga mkono chama chao ambacho kinatajwa kuanzishwa na
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw.Zitto Kabwe, baada ya kuvuliwa nyadhifa
za uongozi ndani ya CHADEMA na kusisitiza kuwa, dhamira yao ni kukuza
demokrasia shirikishi na Serikali inayowajibika.
Kabla
ya mkutano huo, viongozi wa chama hicho walifanya uzinduzi wa baadhi ya
matawi katika Kata ya Igoma, nje kidogo ya jiji hilo.
Post a Comment