Viongozi
wa jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam(JUMIKI) wamefutiwa
mashitaka na mahakama ya wilaya ya Mwanakwerekwe dhidi ya kesi ya
kufanya mkusanyiko bila ya kibali iliofunguliwa Mei mwaka jana visiwani
Zazibar.
Uamuzi huo umetolewa na Hakim Ame Msaraka Pinja baada ya kukamilika
kusikilizwa kesi hiyo na washitakiwa kuonekana hawana hatia katika
mamshitaka yaliokuwa yamefunguliwa na Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar
DPP mapema Mei mwaka jana.
Hakimu Pinja amesema kwa kuzingatia mashahidi wanne upande wa
mashitaka pamoja na washitakiwa wenyewe waliithbitishia mahakama kwamba
katika mkusanyiko wao hawakuwa wakizungumzia mambo ya dini ispokuwa
wakizungumzia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Ameswema kwa msingi huo wqashitakiwa hawakuhitaji kuwa na kibali
chochote cha kisheria kabla ya kuandaa mkusanyiko huo kwa vile walikuwa
wakizungumzia mambo ya Muungano na kwa msingi huo hakuna shitaka
linalowatia hatiani na mahakama imetupilia mbalio dai hilo.
Amesema baada ya mahaka kupitia jalada la kesi hiyo,imeonekana
washitakiwa hawana hatia,ninawaachia huru kwasababu kosa waliloshitakiwa
halikuhitaji kibali cha mufti kabla ya kuandaa mkusanyiko huo”Alisema
Hakimu Pinja.
Hata hivyo Hakimu huyoi wa mahakama ya wilaya ya Mwanakwerekwe
alisema upande wa mashitaka wa Serikali kama haujaridhika na uamuzi wa
mahakama hiyo unaweza kukata rufaa mahakama ya mkoa ndani ya siku 30
tangu kutolewa kwa uamuzi huo.
Washitakiwa katika kes\hi hiyo ni Farid Hadiy Ahmed Mussa Juma Issa,
Haji Sadif Haji,Suleima Juma Suleiman,Fikirini Mjawaliwa Fikirini na
Abdallah Said Ali. .
Washitakiwa walifunguliwa mashitaka kwa kufanya mihadhara ya kiislam
bila kibali cha mufti kinyume cha kifungu cha 6(1)(2) cha kanuni za
kuidhinisha na kuratibu mihadhara zinazotengenezwa chini ya kifungu
15(1) ya sheria Namba 9 ya mwaka 2001 ,kifungu cha 10(1)(c) na kifungu
cha 14(2) ya sheria namba 9 ya mwaka 2001.
Ilidawa bila ya halali Mei 26 mwaka jana majira ya saa 3;30 huko
katika viwanja vya Lumumba wilaya ya Mjini Unguja washitakaiwa walifanya
mihadhara ya kiislam bila ya kuomba kibali cha mufti wa Zanzibar.
Post a Comment