Katika
hali isiyo ya kawaida jioni hii kumetokea vurugu katika uwanja wa CCM
Kambarage mjini Shinyanga wakati wa mchezo kati ya Timu ya Stand United
ya Shinyanga na Polisi ya mkoani Mara ambapo wenyeji wa mchezo huo Stand
United waliibuka washindi kwa bao moja dhidi ya Polisi.
Walioshuhudia tukio hilo wamesema vurugu hizo zimetokea mara baada ya
machezo kuisha,ambapo wachezaji wa timu ya Polisi Mara walipotoka
uwanjani walimfuata refa wa mchezo huo pamoja na wasaidizi wake kutaka
kumpa kichapo,na kufuatia hali hiyo baadhi ya watu waliokuwa katika eneo
hilo wakiwemo wachezaji wa timu ya Stand united waliingia uwanjani
kutaka kumsaidia refa ili asipigwe.
Kati ya watu walioingia uwanjani hapo,aliyekuwa mbele alikamatwa na askari polisi waliokuwa eneo hilo na ndipo vurugu zikaanza na askari hao wanasemekana kuwasaidia POLISI WENZAO wakaanza kurusha mabomu katika eneo la jukwaa kuu ambako alikuwepo pia mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele ambaye pia ni naibu waziri wa madini hapa nchini.
Kufuatia
vurugu hizo baadhi ya watu waliokuwa eneo la jukwaa kuu akiwemo mbunge
wa jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele ambaye pia ni naibu waziri wa
madini wamejeruhiwa katika sehemu mbalimbali za miili yao.
Akizungumza
mara baada ya vurugu hizo naibu waziri wa madini Stephen Masele amesema
vurugu hizo zimetokana na askari polisi waliokuwa wanawasaidia polisi
wenzao yaani timu ya Polisi,walioshindwa kumdhibiti kijana aliyekuwa
anakwenda kumsaidia refa.
Masele
amesema ni vyema TFF ikaaangalia namna ya kupunguza timu za polisi
kwani ziko nyingi sana na wanalindana matokeo yake kusababisha vurugu
leo mjini Shinyanga
Post a Comment