Wakazi wa pembezoni mwa Mto Mbezi wakivuka mto kuelekea upande wa pili.
Mto
Mbezi unaotembea kuanzia Mbezi Kimara kupitia Makongo juu B mpaka Goba
kuelekea Kawe hadi baharini, umekuwa tishio kwa wakazi wa maeneo ya
karibu na mto huo kwani hautabiriki na hata kipindi cha jua unajaa
pasipo watu kujua mvua imenyesha wapi.
“Yaani mto huu ni tishio kubwa kwa wapita njia kwani unaweza kuwa eneo
lako mvua haijanyesha ukajiamini kwa kupita lakini kama imenyesha eneo
lingine ukashangaa maji yamejaa ambayo yanao uwezo wa kumeza mtu, hili
ni tatizo na mbaya zaidi unapanuliwa na wachimba mchanga” alisema mama
Mmoja anayefahamika kwa jina la Mama Adelina.
Wakazi wakiendelea kuvuka mto
Aidha wakazi wa huko wametoa kilio chao kwa serikali kuwatengenezea
daraja kwa ajili ya kuvuka wakati wa mvua kwani ardhi ya huko kupita
njia nyingine imekuwa haifai kabisa kwasababu ya mfinyanzi hasa wakati
wa mvua tatizo ambalo ni la muda mrefu.
PICHA NA GPL
Post a Comment