Mchezaji wa klabu ya soka ya West Brom, Nicolas Anelka amefutwa kazi kwa kosa la utovu wa nidhamu.
Klabu hiyo iliamua kuchukua hatua hiyo baada ya Anelka kutangaza kupitia mtandao wa kijamii kuwa anaacha kazi.
Anelka
alisema kuwa anaondoka katika klabu hiyo baada ya kukosa kutatua
tofauti zilizopo kati yake na Albion kuhusu ishara yake yenye utata
ambayo inasemekana kuwa ya kibaguzi dhidi ya wayahudi.
Mshambuluaji
huyo mwenye umri wa miaka 35, alipigwa marufuku kutocheza mechi tano na
kutozwa faini ya pauni 80,000 na shirikisho la soka Uingereza ,kwa
kufanya ishara hiyo, baada ya kuingiza bao dhidi ya klabu ya West Ham
mwezi Disemba.
West
Brom imechukua hatua ya kumfuta kazi Anelka kutokana na ishara hiyo na
pia kwa sababu ya matamshi yake kwenye mtandao wa kijamii.
Awali aliachishwa kazi mwa muda na Albion, wakati klabu hiyo ilipokuwa inafanya uchunguzi wake binafsi.
Mapema siku ya Ijumaa, Anelka alitangaza kwenye mitandao ya kijamii kuwa anaondoka katika klabu hiyo.
Aliandika:
"kufuatia mazungumzo kati yangu na maafisa wa klabu, kuna masharti
kadhaa ambayo wamenipa kabla ya kujiunga tena na klabu hiyo, Masharti
ambayo siwezi kuyakubali.''
Hata
hivyo klabu ilisema kuwa masharti yaliyotolewa kwa Anelka ni pamoja na
kumtaka awaombe msahama mashabiki , wadhamini na jamii kwa ujumla kwa
athari iliyotokana na ishara yake aliyoifanya Disemba tarehe 28 na pili
akubali kutozwa faini.
BBC SWAHILI
Post a Comment