Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Wananchi 100 wa kata ya Ortumunti wilayani Arumeru kutoka katika vyama mbalimbali vya upinzani wajiunga Chama Cha Mapinduzi


msafara wa katibu  wa ccm wialya ya Arumeru Godfreu Sabuni ukiwa unawasili katika kijiji cha ilikiushing katika mkutano wa adhara
 wamama wa msanja wakiendelea kuserubuka katika mkutano huo






 vijana wakiendelea kuserubuka katika kijiji hicho
 katibu wa vijana wilaya ya arumeru  akiwa Boniface Mungaya akionyesha baadhi ya kadi zilizorudishwa na wanachama wa chadema


 picha ikionyesha baadhi ya wanachama wa liojiunga na ccm wakila kiapo katikati ni aliyekuwa mwenyekiti vijana chadema kata ya orturumenti Thomasi Kivuyo
 mwenyekiti wa vijana chadema kata ya Orturumenti akiwa anatoa mkoano kwa katibu wa siasa uenezi JOnasi Kitoro mara baada ya kukabidhiwa kadi ya ccm
Na Woinde Shizza,Arusha

Jumla ya wananchi 100 wa kata ya ortumunti  wilyani Arumeru  kutoka katika vyama mbalimbali vya upinzani  wamehamia chama cha mapinduzi akiwemo
mwenyekiti wa   vijana wa  chadema kata hiyo .


tukio hilo lilitokea  juzi wakati wa mkutano wa adhara wa chama cha
mapinduzi uliofanyika katika kijiji cha Elikiushing kilichopo wilayani Arumeru mkoani hapa.

Akiongea wakati wa kurudisha  wa kurudisha kadi ya chadema na kukabidhiwa kadi ya ccm mwenyekiti wa vijana wa chadema Thomasi Molel alisema kuwa   ameamua kuchukuwa hatua hiyo mara baada ya kuoana kuwa tangu awe katika chama cha chadema ajapata faida yeyote wala ajaona kitu ambacho wananchi wanafaidika kupitia chama hicho.

Alisema kuwa yeye ni mwanasiasa mzoefu kwani alianza kuingia katika siasa tangu mwaka 1995 na anajua siasa vilivyo hivyo ameamua kuondoka katika chama hicho kwani chadema ni chama ambacho akina democrasia ya
kweli  ambayo inatakiwa iwe nacho kama chama


Alisema kuwa viongozi wengi wa chadema wamekuwa wanatoa ahadi za uongo kwa wananchi  na mbali na hicho pia chama hicho kimekuwa na wasemaji wengi kwani kila kiongozi amekuwa anasema anachotaka badala ya kuwa na msemaji mmoja ambaye ndie atake weza kukisemea chama  .

Aidha alibainisha kuwa katika kata yao  tangu upinzani wameingia madarakani hamna kitu ambacho wamewafanyia wananchi badala yake wamekuwa wakiwachangisha wananchi hela nyingi  bila kufanya
maendeleo yeyote akitolea mfano mchongo wa shilingi elfu mbili ambao ulichangishwa kwa kila mwananchi wa kike na kiume ikisemekana ela hiyo ingeweza kujengea shule lakini adi leo hela hile aijafanya chochote na aijulikani ilipopelekwa

Aliongeza kuwa kingine ni kile kitendo cha kutosomewa mapato na matumizi  ya kata yao tofauti na kipindi ambacho ccm ilikuwa madarakani hivyo.

Kwa upande wake  katibu wa ccm wilaya ya Arumeru Godfrey Sabuni alisema kuwa  wao kama ccm wanawaapokea wananchama hao na pia wamesikia baadhi ya matatizo yao likiwemo la kutosomewa bajeti ya mapato na matumizi kwa kipindi kirefu na aliwaaidi kufuatilia swala hili kwa kwenda
katika ofisi ya mkurugenzi  kufuatilia swala hili.

Aliwasihi wananchi kutofanya makosa katika kipindi hichi kunakoelekea uchaguzi mdogo wa viongozi wa vijiji na vitongoji kwani wakifanya kosa kwa kuchagua viongozi wabovu wataendelea kuteseka  na kata yao haitapata viongozi wazuri.

Aliongeza kuwa haiwezekani kuchagua viomgozi waizi maana mwisho wa siku wanaoumia ni wao wananchi kwani viongozi wao watakula fedha zao
na wao wataendelea kufaidi huku wao wakiwa wanaendelea kuumia ukuwengine watoto wao wakilala njaa
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top